Share this Post

dailyvideo

Bia, soda bei juu


Mwandishi Wetu
SERIKALI imetangaza mabadiliko ya Sheria mbalimbali zinazohusu kudi, zitakazoathiri bei za bidhaa muhimu nchini kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.

Akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2012/13, Dk Mgimwa alisema kodi za bia, vinywaji baridi na vinywaji vikali zitapanda kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Katika ongezeko hilo, soda zitapanda kwa Sh14 kwa lita kutoka Sh69 hadi Sh83, bia yenye kimea pekee itaongezeka kwa Sh62 kutoka Sh248 hadi Sh310 kwa lita wakati bia nyingine zitaongezeka kutoka Sh420 hadi Sh525 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh105.

Vilevile kodi ya mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu zinazolimwa ndani imeongezeka kwa asilimia 75 kutoka Sh145 hadi Sh420, sawa na ongezeko la Sh275 kwa lita.

Kuhusu mvinyo unaotokana na zabibu za nje umeongezwa kodi kutoka Sh1,345 kwa lita hadi Sh1,614 sawa na ongezeko la Sh269 kwa lita.

Vinywaji vikali vimeongezwa kutoka Sh1993 kwa lita hadi Sh2,393 sawa na ongezeko la Sh399.
Bidhaa nyingine iliyoongezwa kodi ni sigara za aina zote, ambazo zile zisizo na kichungi zinazotumia tumbaku ya hapa nchini, imepanda kutoka Sh2,820 hadi 8,210 kwa sigara 1,000.

Wakati zile zenye kichungi na tumbaku ya ndani zimeongezwa kutoka Sh16,114 hadi 19,410 kwa bunda; wakazi zile nyingine zikipanda kutoka Sh29,264 hadi Sh35,117 kwa bunda.
Chanzo: Mwananchi

Posted by Editor on 11:24. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Bia, soda bei juu

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery