Share this Post

dailyvideo

CRDB yajitanua Burundi



na Grace Macha, Arusha
KATIKA kuhakikisha inaingia ipasavyo kwenye ushindani wa kibiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, benki ya CRDB, imeamua kupanua mtandao wake ambapo kwa sasa inafanya utaratibu wa kufungua matawi yake nchini Burundi.
Wanahisa wa benki hiyo kwa kauli moja waliridhia pendekezo hilo lililotolewa na bodi ya wakurugenzi juzi wakati wa mkutano wao mkuu wa 17 uliofanyika jijini hapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema kuwa, wamefanya utafiti wa kutosha kabla ya kufikia uamuzi huo kwani wamebaini kuwa nchini Burundi kuna fursa za kibiashara watakazonufaika nazo.
“Nchini Kenya takribani asilimia 25 ya wananchi wake wamefikiwa na huduma za kibenki, Uganda asilimia 12.4, lakini Burundi hakuna ushindani kwani ni asilimia sita tu ya wananchi wake ndiyo imefikiwa na huduma za kibenki, hivyo ni rahisi kufanya biashara ukilinganisha na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Dk. Kimei.
Pamoja na mambo mengine, wakati wa mkutano huo ulifanyika pia uchaguzi uliowezesha wanahisa, Rose Meta kutoka kwenye kundi la wenye hisa zaidi ya asilimia moja na Juma Abdulrahim na Selina Mkony kutoka kundi la wanahisa chini ya asilimia moja, kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo.
Awali Dk. Kimei akitoa taarifa ya utendaji kwa mwaka 2011, alisema kuwa utoaji wa mikopo uliongezeka kwa asilimia 27 kutoka sh bilioni 1,123 za mwaka 2010 mpaka sh bilioni 1,429 mwaka 2011 ambapo asilimia 30 ya fedha hizo zilienda kwenye sekta ya kilimo.
Chanzo: Tanzania Daima

Posted by Editor on 11:25. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for CRDB yajitanua Burundi

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery