Share this Post

dailyvideo

JUST IN:Hatimaye Dr. Ulimboka apelekwa Afrika ya Kusini kutibiwa mapema leo.


 Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo.

Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo. 

Posted by Editor on 17:19. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JUST IN:Hatimaye Dr. Ulimboka apelekwa Afrika ya Kusini kutibiwa mapema leo.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery