Mwakyembe: Nimemng’oa bosi ATCL kwa ufisadi

ASEMA WANAOUNUNG’UNIKA WAKO HURU KUJIONDOA
Fidelis Butahe
SIKU nne baada ya Kung’olewa Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe Ameamua kuanika Tuhuma za Ufisadi Zinazodaiwa Kufanywa na kigogo huyo.Miongoni mwa Tuhuma hizo ni kuingia Mkataba wa kununua Ndege bila Kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na kununua sare 15 za watumishi wa Ndege kwa Dola 50,000 za Marekani.
Juni 5, Dk Mwakyembe Alitengua Uteuzi wa Chizi na kumteua Rubani wa Muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro Kukaimu Nafasi hiyo, akisema Uteuzi Ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma: Chanzo cha Habri Gazeti la Mwananchi. http://mwananchi.co.tz




