MWANANCHI ALIYEOKOLEWA NA ASKARI WA MUHIMBILI KUTOKA MIKONONI MWA MADAKTARI WENYE HASIRA
Askari wa Hospitali ya Muhimbili, wakimuokoa mwananchi aliyenusurika kwa kipondo cha aja kutoka kwa Madaktari waliomshuku kuwa jamaa huyu ni mmoja kati ya watu wa usalama wakati akikatiza anga hizo walipokuwa katika harakati za kumsaidia kiongozi wao, ambapo walimvamia na kuanza kumshambulia kabla ya kuokolewa na askari hao.
Hata hivyo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari jana alionya juu ya wananchi kuchukua sheria mikononi bila kufuata sheria kwa kuwa zinaweza kuleta madhara hata kwa ndugu zao kwani kachelo huyo alikuwa kazini na ndiye aliyefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa suala la Dk. Steven Ulimboka linashughulikiwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuletwa hospitalini hapo.
Picha kwa hisani ya Full Shangwe
Posted by Editor
on 19:41.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
Huyo ni mwanachi tuu.. Au ni mwananchi Kachelo??? Haijawa clear hapo... Sidhani kama ni sahihi kuonesha kuwa haata nyie mnaficha... Inaweza kuibua hisia tofauti kwa waatu... Huyo ni Kachero, watu wakijua ni mwananchi tu, hisia ni tofauti na wakijua ni Kachero! Au ndo uandishi wenyewe huo labda... Hi hi hiiiii...!!
huyu wala sio mwanamchi bali ni afisa wa polisi.
Nakupa pole afande Mokily kwa tukio hilo, ila madaktari waliompiga wanastahili kuchukuliwa hatua hakuna kuwanyamazia hawa