Share this Post

dailyvideo

News Alert: Serikali kuwakaanga Madaktari kesho



Yasema litakalo kuwa na liwe

Na Dotto Kahindi-Thisday Magazine
SERIKALI imesema kesho itatoa tamko la mwisho kuhusu mgomo wa madaktari baada ya Chama cha Madaktari (MAT) kukaidi amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kusitisha mgomo wao kwa kutangaza kusitisha mgomo huo kupitia vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja ya mbunge wa CCM Jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi aliyeitaka serikali kutoa tamko juu ya mgomo wa madaktari badala ya kutumia mahakama kuzuia mgomo huo huku wagonjwa wakindelea kuumia kwa kukosa huduma.
 “Kesho tutatoa kauli ya mwisho kwa madaktari, litakalo kuwa na liwe” alisema Pinda
Jana Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi imekionya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kuhusu utekelezaji wa amri yake ya kusitisha mgomo wao na kukiagiza rasmi kutangaza kusitisha mgomo huo kupitia vyombo vya habari, hadi Julai 24, 2012.
Onyo na amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Sekela Moshi kwa Rais wa MAT akirejea amri aliyoitoa Ijumaa iliyopita akikiagiza chama hicho na wanachama wake kutoitisha mgomo wala kushiriki katika mgomo huo.

Jaji Sekela alitoa amri hiyo kufuatia maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Serikali ikiomba mahakama isikilize na kutoa uamuzi wa upande mmoja wa kuzuia mgomo huo kwa muda kusubiri usikilizwaji wa pande zote wa maombi hayo.

Amri hiyo ya jana ilikuwa inakazia nyingine ambayo ilitolewa Ijumaa iliyopita, siku ambayo chama hicho kilitangaza kuanza kwa mgomo siku inayofuta.
Hata hivyo amri hiyo haikutekelezwa na chama hicho na kulikuwepo na madai kwamba viongozi hawakupatiwa nakala ya amri hiyo na hivyo Taasisi ya  Mifupa Muhimbili (MOI) jana ikalazimika kutangaza rasmi kusitisha baadhi ya huduma zake kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea nchini na kushika kasi zaidi katika hospitali za rufaa za KCMC, Bugando na Mbeya

Posted by Editor on 15:07. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for News Alert: Serikali kuwakaanga Madaktari kesho

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery