Tyson Chandler Nyota wa Kikapu Nchini USA Atua Jijini Dar es Salaam
Picha Juu Tyson akiwa Don Bosco wakati wa mafunzo kwa vijana wadogo/watoto wa
mitaani na picha nyingine ni Mkurugenzi wa Michezo na Ushirikiano wa
UNICEF USA akiwa na Magesa/TBF-VP.
---
Nyota wa Kikapu, Tyson Chandler Mchezaji mahiri wa kikapu toka Marekani
anayechezea timu ya New York Knicks kama "center" na pia anachezea timu
ya Taifa ya Marekani yuko jijini Dar Es Salaam kwa ziara maalumu.
Tyson yumo kwenye timu ya Taifa ya Marekani iliyotwaa medali ya dhahabu
katika mashindano ya Olimpiki ya 2012 yaliyomalizika London na alicheza
michezo yote.
Tyson ambaye msimu huu wa ligi ya NBA iliyoisha alichaguliwa kuwa
mchazaji bora mzuaji/Mlinzi (NBA Defensive Player of the year) pia ni
balozi wa heshima wa UNICEF.
Katika ziara ya Dar amefanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo
kutoa mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo/ watoto wa mitaani katika
viwanja vya Don Bosco.
Tunamshukuru sana Tyson na pia tunawashukuru UNICEF kwa ushirikiano wao.
Phares Magesa
Makamu wa Rais,
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF).