Share this Post

dailyvideo

CCM YATOA TAMKO MAUAJI YA KUTISHA MWANDISHI WA HABARI yaliyotokea mkoani iringa.


Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi Nape Moses Nnauye akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari jijini Mwanza leo.

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Itakumbukwa tarehe 02/09/2012 katika operesheni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwanahabari mzoefu Ndg. Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa  askari watatu wa kuzuia fujo. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. Tunatoa wito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote - ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu Daudi Mwangosi.
Vyama vya siasa na wanasiasa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu Utawala wa sheria ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo nchini uliojengwa kwa muda mrefu kutokana na misingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu. Kauli hiyo imetolewa leo na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Mnauye jijini Mwanza leo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi wa Chanel Ten Mkoani Iringa wakati wa vurugu za polisi na wafuasi wa Chama cha CHADEMA mwezi September 2 mwaka huu 2012
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Taifa.

Posted by Editor on 19:32. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for CCM YATOA TAMKO MAUAJI YA KUTISHA MWANDISHI WA HABARI yaliyotokea mkoani iringa.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery