Hii ni Bab Kubwa: DJ Choka aamua kusheherekea birthday yake barabarani mitaa ya Morocco na watoto wa mitaani
![]() |
| Dj Choka |
Dj wa wasanii na blogger maarufu hapa Tanzania Hugoline Martin anaefahamika zaidi kama Dj Choka leo Sept 19, 2012 ni siku anayokamilisha miaka 28 tangu ameanza kupumua.
Akiongea na Leotainment amesema anafuraha kubwa kuweza kuifikia siku ya leo na ameamua ku celebrate tofauti kwa kununua juice na keki kwa ajili ya kwendavyo kusheherekea na watoto wa mtaani wanaopatikana maeneo ya Morocco Bagamoyo road.
![]() |
| Dj Choka alivyosheherekea birthday yake na watoto wa mitaani |
Dj Choka amesema sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na ndoto iliyomjia usiku wa leo ambapo aliota anakula na watoto yatima, so akajiuliza kwanini hii ndoto imekuja siku kama ya leo, na ndoto inamaana gani? Ndipo alipoamua kufanya kitu hicho. Choka amesema hana mpango wa kufanya party nyingine yoyote kwa leo kama ambavyo wengine hufanya kwa kualika friends na kula bata za kutosha.








