Mgomo wagawa madaktari
Jumuiya ya Madaktari nchini imesema madaktari walioomba radhi kwa kushiriki katika mgomo uwametumiwa kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha huduma za afya pamoja na maslahi ya watumishi.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Godbless Charles, alisema jana kuwa madai ya madaktari sio tukio bali mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslai ya watumishi kwa ujumla, jambo hilo tumelilaani kwani madai yetu ni ya msingi,” alisema.
Akizungumzia suala la madaktari wa mafunzo kwa vitendo (Interns), alisema Julai10, mwaka huu, Baraza la Madaktari Tanzanai (MCT) lilitoa taarifa kwa umma kuwa limesitisha leseni za muda kwa madaktari hao na na kuahidi kuwaita kuita na kuwahoji mmoja mmoja baada ya uchunguzi.
Charles alisema cha kushangaza mpaka sasa miezi miwili imepita na bado haijafamika ni lini wataitwa katika baraza hilo kwani muda unazidi kwenda.
Alisema MCT inatakiwa kutekeleza kwa haraka majukumu yake kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki za madaktari hao.
habari NA BEATRICE SHAYO
CHANZO: NIPASHE




