TAMKO LA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF), KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI
![]() | ||
| Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena |
UTANGULIZI:
1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.
2.Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
3.Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.
4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.
5.Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.
6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.

MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF
Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:
1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.
2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.
3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

4.Tunasema hivi
kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au
nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani
kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba
hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.
5.Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.
6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

7. Vitendo vya
aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa
ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea
katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia
badala ya kuwa walinzi wa raia.
8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.
9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.
IMETOLEWA NA:
NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012

Waandishi wa habari katika hili tamko lenu manataka safu ya uongozi wa polisi uwajibike,sawa lakini mimi nakwenda mbali zaidi,kwamba kwa kuwa polisi wamefanya mengi yafananayo na haya hata wakiwajibika hao viongozi bado swala la uozo litakuwa palepalee.Mimi naona yafuatayo ili serikali kuficha aibu yake,waziri mambo ya ndani na wa utawala bora wote waungane na kuwajibika,jeshi la polisi sasa ni wakati mwafaka wa kuundwa upya ili lipatikane jeshi kweli la polisi litakalo kwenda na wakati huu wa sasa wa vyama vingi,hawa bado wapo kulekule kwenye mfumo wa chama kimoja na hapa hakuna cha ajabu mbona mwaka 1964 jwtz baada ya kuboronga kwa sana liliundwa upya nini cha ajabu bwana?hakuna polisi yeyote aekwenda na wakati huu wa sasa, na kama wapo haya yanayotokeaa kila siku yasingetokea hata siku moja,labda kama wanajeshi wangepelekwa tungesema ndiyo maana wao hujifunza kuua tu na si vinginevyo lakini na wao hata huko vitani hawajawahi kuua kwa namna hiyo hata kama anaeuawa ni adui.watanzania wengi wameisha poteza maisha kwa staili hii na hakuna chochote kinafanyika badala ya kula na kulala kwa mishahara ya watanzania na inageuka kuwaua wenyewe tena hapana polisio iundwe upya hata kama kwa kufanya hivo ni maamuzi magumu kiasi gani na kwa gharama gani cha msingi tupte tanzania polisi wazuri, waelewa,weledi kwa kazi yao, shupavu,wa kutathimini jambo la kufanya kabla ya kufanya,wa kuheshimu wanaowatumikia,wa kwenda na wakati kwa kadiri mazingira yatakavyo badilika.Wakati huu wa mpito kazi zote za polisi zifanywe na polisi jeshi ambao nina uhakika watafanya vizuri mno wakisaidiana na wanajeshi wastaafu,hadi hapo jeshi lenyewe litakapo kuwa limeundwa nakumaliza mafunzo ambayao yatafanywa nje na ndani kulingana na daraja la huyo polisi mpya na baadae Raisi atateua mkuu wa polisi aliyetoka chuo akiwa ameiva na ana mtazamo mpya na wliokuwa wameshikilia wafanye nao miaka mitano nakisha wawaachie waendelee kwa matazamio ya miaka kadhaa ndipo waendelee wenyewe sasa.Hapo yafuatayo yatakomeshwa kabisa,mauaji kwa raia,ruhwa miongoni mwao kwa secta mbalimbali zinazofanywa na polisi,Ajali za barabarani zitaisha kabisa kwa kuwa magari mabovu na madereva walevi hawatapita barabarani hata siku moja na kama ni ajali basi kweli kwa bahati mbaya sana,kesi zote mahakamani zita kwenda haraka sana,tutainua uchumi wa nchi hii kwa nama moja au nyingine na mengine mengi yatafanikiwa kupitia njia hii ya kuundwa upya jeshi la polisi.Wanaosikia hili na wasikie na kulitendea kazi kinyume cha hapo litakuja lingine kubwa zaidi ya hili la mwangosi kuuawa peke yaketu hawa jamaa watakuja kuua watu wengi na hasa wakati wa harakati za uchaguzi wakati si kweli kwamba kutawanya watu kwenye maandamano lazima utumie risasi za moto hata hizo za baridi kwa lipi?kwa nini isiwe virungu kwa kupiga sehemu stahiki na matu akajisalimisha mwenyewe?sikubaliani kabisa mimi hata na kwenda na bunduki kwenye maandamano tena pengine ni ya wanafunzi tu au waandamanaji hawana hata silaha iitwayo karatasi au pini.Tubadilike kuanzia sasa na kifo cha Daudi Mwangosi kiwe kielelezo cha mabadiliko katika nchi hii dhidi ya jeshi la polisi, vinginevyo historia itatuhukumu sote.
TEF tamko lenu nilitegewa kuwa kali kuliko lile ta IPC na MBPC. japo piga mgomo wa muda fulani kutoshirikiana na polisi kama alama ya kutoa kilio chenu kwa umma.