DAR LIVE YACHANUA NA MSAKO WA THE MIC KING, TMK WANAUME NA EXTRA BONGO...!!!
SHINDANO la kumtafuta Mfalme wa Mic (The Mic King), jana liliendelea katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem na kuwapata wawakilishi 12 wa wilaya ya Ilala huku burudani ya kufa mtu ikiporomoshwa na kundi la Wanaume TMK na Bendi ya Extra Bongo.
Memba mzee wa kundi hilo, Bibi Cheka (kushoto) akimwaga mistari jukwaani. Kulia ni Temba.
Majaji wa The Mic King, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (kushoto), John Dilinga ‘DJ JD’, na Sister P wakifuatilia shindano hilo.
Msanii anayesumbua na songi la Mwanayumba ndani ya gemu la Bongo Fleva, Chegge Chigunda, akimsaka ‘Mwanayumba wake’ jukwaani.
Zao jipya la Kundi la TMK Wanaume, mwanamuziki Getruda, akionyesha uwezo wake jukwaani.
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA/GPL)












