Share this Post

dailyvideo

JAJI MKUU ZIARANI MAREKANI


 Jaji Mkuu wa Tanzania  Mhe.Mohamed Othman Chande yuko ziarani nchini Marekani ziara ambayo imejumuisha Majaji Wakuu wengine kutoka Afrika Kusini,Ghana,Namibia,Zanmbia,Malawi,Kenya,Uganda na Msumbiji, Ziara hii ya aina yake imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na madhumuni yake makubwa ni kujionea jinsi mfumo wa Sheria na Utoaji Haki katika mahakama vinafanya kazi pamoja na maeneo ya Utawala Bora. Katika ziara hii Jaji Mkuu Chande ametembelea mahakama ya Rufaa ya Marekani jijini Washington DC pamoja na Chuo Endelevu cha Majaji Chicago na leo hii alionana na Mhe.Hilary Clinton, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani pamoja na Majaji wengine waalikwa na kuwa na mazungumzo nae katika Wizara ya Nje ya Marekani Washington DC.
Mhe.Mohamed Othman Chande PIA alipata wasaa wa kutembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC.Katika picha Mhe. Chande akipokelewa na Bw. Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC na pia akisaini kitabu caha wageni Ubalozini hapo. Mhe.Chande akiwa na Bw.Suleiman Saleh mara baada ya kumaliza ziara yake Ubalozini.

Posted by Editor on 12:01. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JAJI MKUU ZIARANI MAREKANI

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery