Share this Post

dailyvideo

SULTANI QABOOS WA OMAN AMTUNUKU NISHANI YA HESHIMA RAIS JAKAYA KIKWETE


Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said (kulia)  akimtunuku Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.
Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman jana jioni katika kasri ya AL Alam, Jijini Muscat Oman jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku tatu. Picha na Freddy Maro.

Posted by Editor on 12:34. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SULTANI QABOOS WA OMAN AMTUNUKU NISHANI YA HESHIMA RAIS JAKAYA KIKWETE

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery