JUST IN: TFF YAMWENGUA MUHIDIN NDOLANGA
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imetangaza kumwondoa
Muhidin Ndolanga kwenye Kamati ya uchaguzi ya Chama cha Waamuzi nchini (FRAT) kwa
kushindwa kuzingatia Katiba na taratibu za uchaguzi mkuu wa chama hicho ambao
ulifanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
Ndolanga ambaye mwaka jana alisimikwa kuwa mjumbe wa heshima wa TFF, ameenguliwa kuwa mwenyekiti wa Frat baada ya kukiuka Katiba ya FRAT ikiwa ni pamoja na maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya
TFF chini ya Deo Lyato iliyomtaka kusitisha uchaguzi huo kufatia baadhi ya taratibu
kutokamilika jambo ambalo kiongozi huyo alilipuzia na kuendesha uchaguzi huo.
Kufuatia hali hiyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeamua kumchukulia hatua za kinidhamu
kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi ibara ya 26 (8) kumwondoa kwenye kamati hiyo ikiwa
ni pamoja na kumtaka Katibu mkuu wa TFF kumwasilisha kwenye Kamati ya Nidhamu
ya Shirikisho hilo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaa, Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Deo
Lyato alisema kuwa uchaguzio huo uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma ni batili
pamoja na viongozi wote waliochaguliwa ni batili na hawatumbuliki na TFF kwa kuwa
haukuzingatia kanuni.
"Uchaguzi wa FRAT uliofanyika Novemba 17 Dodoma ni batili kwa kuwa haukuzingatia
kanuni za uchaguzi za wanachama na maagizo ya TFF," alisema Lyato.
Alisema baadhi ya taratibu zilizokiukwa na Ndolanga ni kuwaruhusu wagombea ambao
tayari walikuwa wameenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika uchaguzi huo kwa
kutokuwa na sifa.
Wagombea hao ni Omari Abdulkadir, Sudi Abdi pamoja na Ruvu Kiwanga ambao wawili
kati yao walibuka na ushindi katika uchaguzi huo.
Hatahivyo Lyato alisema pia watu hao pia watafikishwa katika kamati ya Nidhamu ya TFF
kwa mujibu wa ibara ya 26(8) ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa shirikisho hilo
kwa hatua za kinidhamu.




