Share this Post

dailyvideo

MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI, WASILIANA NAO SASA KWA NAMBA +255 757 361 266



Wanafunzi wa mafunzo ya muziki wakiwa kwenye somo la matumizi ya viungo vya mwili katika kutengeneza midundo, yaani “body percussion’ picha zote na AMTZ

****************************

ACTION MUSIC TANZANIA (AMTZ) YAANZA KUTOA MAFUNZO YA UPIGAJI WA ALA ZA MUZIKI
‘MUSIC DECEMBER 2012’

Action Music Tanzania (AMTZ) ni asasi iliyosajiliwa na BASATA na kupewa namba ya usajili BST/4733, imeanza kutoa mafunzo ya upigaji ala za muziki kwa watu mbalimbali katika kipindi hiki cha likizo, yanayoitwa ‘Music December 2012’

Mafunzo hayo ya upigaji wa ala za muziki ni kwa watu wote ambao hawajaingia na wale waliokwishaingia katika tasnia ya muziki lengo likiwa ni kuwafundisha na kuwajengea uwezo kimuziki (muziki kama taaluma), ambapo mwanamuziki atajengewa uwezo wa kutunga, kuandika, kusoma na kucheza ala kitaalam na jukwaani yaani ‘Live’

Mafunzo haya yanafanyika kuanzia mwezi disemba ili kutoa fursa kwa wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi na sekondari kujiunga, pia kuwapa nafasi watu walioko makazini kutumia fursa hii kujifunza muziki.

Mafunzo ya upigaji ala za muziki kwa vitendo yatahusisha ala za muziki kama Kinanda (piano,keyboard), Ngoma aina ya Konga, djembe na za mapipa, Tarumbeta ya Bb, Saxophone ya Eb (alto sax), Gitaa la sauti ya juu (solo, rhythm) na chini (bass), Seti ya Ngoma za Kimagharibi (drum set/kit) na Matumizi ya viungo vya mwili katika kutengeneza midundo, yaani “body percussion’

Mafunzo hayo yataambatana na nadharia ya Music ambapo mwanafunzi atajifunza namna ya kuandika, kusoma na usikivu yaani ‘music writing, sight reading and ear training’

Mafunzo yanafanyika katika ofisi za Action Music Tanzania Mwenge, maeneo ya ITV, karibu na Maryland bar – Shule ya Msingi Mwenge na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho (FPA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mafunzo yanatolewa na walimu wa muziki kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na kutoka kwenye bendi na taaisis nyingine za muziki hapa nchini.

Fomu za usajili zinapatikana ofisi ya AMTZ karibu na Shule ya msingi Mwenge kwa shilingi za kitanzania 2,000/= tu. Njoo ujifunze kupiga ala za muziki kwa muda mfupi na kwa bei nafuu.

Imetolewa na
Mandolin Kahindi
Katibu Mtendaji-AMTZ
Tell: +255 757 361 266

Posted by Editor on 15:53. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI, WASILIANA NAO SASA KWA NAMBA +255 757 361 266

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery