Share this Post

dailyvideo

Vijana wasiozidi miaka 14 Marekani wamuua mwanadada baada ya kuwaambia acheni kuomba sigara ‘katafuteni kazi’

Polisi nchini Marekani imesema wavulana wawili wenye umri wa miaka 13 na 14 wanashitakiwa kwa mauaji mabaya baada ya kumpiga risasi mwanamke mmoja mkazi wa Pennsylvania, waliyekuwa wame-mtageti , baada ya mwanamke huyo kuwaambia wakatafute kazi.
Polisi wameongeza kuwa katika tukio hilo jumla ya vijana watatu wanatuhumiwa kwa mauaji ya mwanamama huyo ambaye walimvamia, baada ya kuwaambia katafuteni kazi, alipoona wanambugudhi mchumba wake wakimuomba sigara.
Kituo cha Polisi cha Beaver Falls kimefungua mashitaka dhidi ya Todavia Cleckley na Marcus Velasquez wenye umri wa miaka 14 na Kyle Goosby Jr. mwenye miaka 13, kwa uhalifu wa mauaji ya Kayla Peterson (22).

Posted by Editor on 00:23. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Vijana wasiozidi miaka 14 Marekani wamuua mwanadada baada ya kuwaambia acheni kuomba sigara ‘katafuteni kazi’

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery