Share this Post

dailyvideo

ANGALIZO KALI : JIHADHARINI NA UTAPELI HUU KUHUSU MIKOPO


Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Nimelazimika Kuandika Ujumbe huu kwaajili ya kuutarifu umma wa watanzania mara baada ya kupokea Ujumbe mfupi wa Sms kutoka Kwa rafiki yangu Mroki Mroki juu ya Kuingiliwa kwa akaunti ya Facebook na kuandika Ujumbe wa Kitapeli.

Huu ni Ujumbe ulioandikwa katika Ukurasa wa Rafiki yangu Mroki Mroki katika Ukurasa wake wa Facebook ukijaribu Kuwaaminisha watanzania Juu ya Mikopo inayotolewa na Kutumia Mbinu mbalimbali ili kuweza kutapeli watu.

Baada ya kuona Ujumbe Huo Mroki Mroki aliamua kuwajulisha Baadhi ya Rafiki zake kuweza kumsaidia Kuwataarifu wengine kuhusu ujumbe kuwa Siyo Mroki Mroki aliyeandika Ujumbe huo bali ni Matapeli wa Mtandaoni walioweza kuingilia akaunti yake ya facebook na kuweza kuandika Ujumbe huo wakijaribu kuwaaminisha Umma kama wanatoa Mikopo Bila Riba.
Napenda Kuchukua Nafasi hii Kuwataarifu watanzania kuwa HUU NI UTAPELI MSITHUBUTU KUTUMA PESA MTAIBIWA.
USHAURI WANGU KWA WATUMIAJI WA MITANDAO HII PAMOJA NA BARUA PEPE.

Tuwe na Utaratibu wa Kubadilisha mara kwa mara Namba au Maneno ya Siri tunayotumia katika Kuingilia katika akaunti zetu za barua pepe au akaunti zetu za facebook .Kwa kufanya Hivi tunaweza kuzuia watu kuingilia Akaunti zetu Kwa kiasi kikubwa .

Posted by Editor on 18:54. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for ANGALIZO KALI : JIHADHARINI NA UTAPELI HUU KUHUSU MIKOPO

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery