Wednesday, 16 April 2014

MWANAMKE WA KIGHANA AKAMATWA NA KILO 10 ZA HEROIN AKITOKEA TANZANIA


Mfanyabiashara mwanamke wa Kighana (pichani) amekamatwa na kilo 10 za Heroin wakati akitokea Tanzania. Mercy Agyeman Prempeh (36) amekamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kotoka wakati akitokea Tanzania. Polisi walimtaka mwanamke huyo kutambua mizigo yake uwanjani kutokana na sehemu aliyokuwa anatokea yaani Tanzania. 

Baada ya kuhojiwa na polisi alidai kuwa rafiki yake wa Kitanzania ndiye aliyempa mzigo huo ampelekee mtu asiyejulikana anayeishi katika jiji la Accra kwa ada ya Dola za Kighana 2,500. Amedai mwenye mzigo alitakiwa akutane nae hapo airpot na kumpatia kiasi hicho cha fedha lakini anaamini amengia mitini baada ya yeye kukamatwa.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

Sample Text