Share this Post

dailyvideo

WAZAZI KAUNTI YA KIRANGA MKOA WA KATI NCHINI KENYA WAANDAMANA BAADA YA MWALIMU KUMCHAPA MWANAFUNZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE

Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.
Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.
Wazazi hao waliandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.


Hata hivyo polisi waliweza kumkamata mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.


Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.

Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu kumchapa kwenye kisogo.

Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia kile wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo walitaka mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo hicho cha kumchapa mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini Kenya.

Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine.

Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.

BBC

Posted by Editor on 07:59. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WAZAZI KAUNTI YA KIRANGA MKOA WA KATI NCHINI KENYA WAANDAMANA BAADA YA MWALIMU KUMCHAPA MWANAFUNZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery