Share this Post

dailyvideo

JE WAJUA KUWA MVINYO HAUNA MANUFAA KWA AFYA YAKO?


Kunywa mvinyo haisaidii afya yako
Je umekuwa ukibugia mvinyo ili ili ukusaidie kiafya?
Watafiti wanadai kuwa mvinyo mwekundu (Red wine) hauna manufaa kama ilivyodhaniwa kuwa nayo kwa moyo wa binadamu.
Wanasayansi nchini Italia wamekuwa wakichunguza wenyeji 800 kutoka eneo la Chianti maarufu kwa unywaji wa mvinyo mwekundu nchini humo na kubaini kuwa mvinyo huo hauna faida yeyote kama ilivyodhaniwa awali.
Aidha watafiti hao wamegundua kuwa kirutubisho cha mvinyo huo ''Resveratrol'' hakizuii maradhi ya moyo wala kurefusha maisha ya wale wanayoikunywa mvinyo huo mwekundu.

Prof Richard Semba

"Hadi kufikia hapa tulipo sifa iliyolimbikiziwa kiungo cha Resveratrol eti kuwa inafaida kubwa kwa siha ya binadamu si kweli. Hakuna udhibitisho wa kisayansi unaounga mkono sifa hizo za faida kwa afya"
Kufuatia ripoti yake Professa Semba wakfu wa wagonjwa wa moyo nchini Uingereza tayari umeanza kufanya utafiti wake kupata ukweli kuhusu kiungo cha resveratrol.
Utafiti huo hautakuwa wa kwanza.
Utafiti umefanywa mara nyingi nchini Ufaransa kujaribu kutanzua kitendawili cha matukio machache sana ya maradhi ya moyo miongoni mwa wenyeji nchini Ufaransa ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi ilihali asilimia kubwa ya
wafaransa ni waraibu wa vyakula vya kukaangwa kwa mafuta mengi na wanywaji wa mvinyo.
Utafiti wa awali umekuwa ukiashiria kuwa unywaji huo wa mvinyo mwekundu ulaji wa chocolate na matunda labda ndiyo huzuia maradhi ya moyo.
Watafiti waligundua kuwa kiungo cha Resveratrol ndicho kibwagizo katika vyakula hivyo vyote na hivyo kuipigia debe kuwa ndiyo sababu ya afya nzuri ya wafaransa.
Kunywa mvinyo haisaidii afya yako
Lakini Prof Richard Semba, kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins ameshindwa kuthibitisha hilo.
Aliwaongoza madaktari watafiti wa maradhi ya moyo kuwachunguza wakongwe 783 kutoka mji wa Tuscany ambao walitoa maelezo kuhusu siha zao vyakula wanavyokula na kunywa na hata mkojo ili kufanyiwa utafiti na kwa zaidi ya kipindi cha miaka 9.
Katika kipindi hicho cha miaka 9 wakongwe 268 walioshiriki katika utafiti huo waliaga dunia 174 walipata maradhi ya moyo na wengine 34 walipatikana wameathirika na ugonjwa wa saratani.
Resveratrol haikuonekana kusaidia katika matukio hayo yote na hivyo kutilia shaka faida yake mwilini.
Daktari wa moyo nchini Uingereza Maureen Talbot,anasema licha ya ripoti hiyo wakfu wa magonjwa ya moyo nchini Uingereza hautabadilisha ushauri wake kwa umma kuwa watu waendelee kula mboga matunda na nafaka.


BBC SWAHILI

Posted by Editor on 19:57. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JE WAJUA KUWA MVINYO HAUNA MANUFAA KWA AFYA YAKO?

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery