Share this Post

dailyvideo

KUWAONA STARS WA WAPYA v/s ZIMBABWE KIINGILIO 5,000/= Kiingilio cha chini cha mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.


Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.

Tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi hiyo katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam, na uwanja siku ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij inatarajia kurejea jijini Dar es Slaam kesho (Mei 14 mwaka huu) kutoka Mbeya kuendelea na maandalizi ya kuikabili Zimbabwe.

Posted by Editor on 20:50. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for KUWAONA STARS WA WAPYA v/s ZIMBABWE KIINGILIO 5,000/=

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery