Share this Post

dailyvideo

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA UFUTA CHA TAKEMOTO, NAGOYA JAPAN NA BAADAE AHUTUBIA WASOMI JAPAN UMUHIMU WA VITEGA UCHUMI KWA MAENDELEO YA AFRIKA


 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta cha  Takemoto, Akira Ogawa
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyoanza kuandaliwa kuelekea katika mashine za kukamua mafuta. Hapa ni hatua ya kwanza zinaposhushwa mbegu hizo na kuingia moja kwa moja kwenye mitambo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyosafiri hadi kufika katika Kinu cha kuzisaga hadi kupatikana mafuta hayo, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mafuta ya ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya hayo cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mbegu za ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan
 Wakiendelea kutembelea kiwanda hicho.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu kiwanda hicho kinavyofanya kazi hadi kupatikana mafuta ya Ufuta, wakati walipofika kiwandani hapo kujionea kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji, jana Mei 22, 2014.
   akiendelea kupata maelezo....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona (wa pili kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakiongozana wakati walipokuwa wakielekea kutembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo Japan, jana Mei 22, 2014, akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Japan.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wanachuo Watanzania, wanaosoma katika Chuo hicho baada ya kumalizika kwa Muahadhara huo jana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa muhadhara katika Chuo Kikuu cha Taaluma ya Sera 'GRIPS' wakati alipoalikwa kwenye muhadhara huo uliofanyika chuoni hapo Jijini Tokyo Japan, jana Mei 23, 2014.
   Baadhi ya wanachuo kutoka mataifa mbalimbali wa Chuo hicho waliohudhuria Muhadhara huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati alipokuwa akitoa muhadhara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Japan, waliohudhuria Muhadhara huo baada ya kumalizika kwa muhadhara huo katika Chuo Kikuu cha Taaluma ya Sera 'GRIPS' Jijini Tokyo Japan, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachuo Watanzania wanaosoma katika Chuo hicho cha  Taaluma ya Sera 'GRIPS' Jijini Tokyo Japan, jana Mei 23, 2014, baada ya kumalizika kwa muhadhara huo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
---
Na Mwandishi Maalum, Tokyo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amesema nchi zinazoendelea hususan za Kiafrika bado zinahitaji uwekezaji zaidi vitega uchumi kutoka nje  (FDIs) ili kupata maendeleo ya haraka na  kuondokana na umaskini.
Dkt. Bilal ameyasema hayo leo (Mei 23, 2014) wakati akitoa muhadhara kuhusu Mtazamo wa Nchi Zinazoendelea  na  Changamoto za Uwekezaji Vitega Uchumi  vya Nje na Hatma yake katika Kuondoa Umasikini kwa  kutumia  mfano wa Tanzania ulioandaliwa na  Taasisi ya Uchanganuzi wa  Sera (GRIPS)  mjini  Tokyo.
Alisema Afrika inahitaji misaada zaidi itakayosadia kukuza teknolojia itakayowawezesha Waafrika kuvuna  maliasili ambazo hazijavunwa. Aliongeza kuwa hii ndiyo njia pekee itakayoliwezesha Bara la Afrika kuongeza mapato na kuchangia maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.
Alisisitiza  kuwa uwekezaji unaohitajika zaidi ni katika sekta za  za madini, mafuta na gesi, kilimo na vyanzo vingine vya nishati kama vile nishati ya jua na upepo. Alisema sekta hizo ndizo zinazohitaji teknolojia ya kisasa kutoka mataifa yaliyoendelea ili kurahisisha uvunaji wake.

Wakichangia hoja hiyo, wanafunzi wa chuo hicho walihoji namna Tanzania inavyojiandaa kuhakikisha upatikanaji wa mafuta na gesi hauwezi kuathiri amani na utulivu wa nchi yetu. Makamu wa Rais aliwaeleza kwamba utafutaji, uchimbaji na usambaji unafanyika katika misingi ya uwazi ili Serikali na  kila mwananchi aelewe ni kwa namna gani atakavyonufaika na rasimiali hiyo.

Posted by Editor on 17:42. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA UFUTA CHA TAKEMOTO, NAGOYA JAPAN NA BAADAE AHUTUBIA WASOMI JAPAN UMUHIMU WA VITEGA UCHUMI KWA MAENDELEO YA AFRIKA

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery