MMOJA WA WASHIRIKI WA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA APOTEA, SEMINA ZAENDELEA.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kama kawaida wanakijiji walianza siku kwa kufanya
mazoezi ya viungo ili kuweka miili yao sawa tayari kukabiliana na shughuli za
siku hiyo. Baada ya mazoezi kumalizika wanakajiji walibaini mmoja wao ametoweka katika mazingira
ya kutatanisha bila kujua ameelekea wapi. Hofu ilitanda katika kijiji cha
Maisha Plus huku wanakijiji wakijiuliza kimetokea nini kwa mwenzao Anna
Mwanilyela Chrisant kutoka Katavi kwani wengine walidhani amekufa, wengine
walidhani ametoroka, wengine walidhani ni mchezo umefanyika na baadaye anaweza
akarudi na wengine walidhani
amechukuliwa na Epheta Msiga ambaye huonekana kwa nadra sana hapo kijijini.
Kuonekana kwake ni ishara ya mwanakijiji mmoja kuaga mashindano hayo. Kwa kweli
wanakijiji wote hawakuwa na jibu kamili ya wapi mwanakijiji huyo ameelekea.
Hofu ilitanda zaidi pale askari polisi wapofika katika kijiji cha Maisha Plus
baada kupewa taarifa ya kupotea kwa mwanakijiji huyo na kufanya mahojiano na
uongozi wa kijiji ili kupata taarifa zitakazosaidia kumtafuta mwanakijiji
aliyepotea.
Mahojiano yalifanyika
na mwanakijiji anayedhaniwa kapotea katika mazingira ya kutatanisha na kumkuta
katika hali ya usalama na alikuwa na haya kusema ‘washiriki wasiwe na hofu
kwani kilinifanya leo niage mashindani ni kutokana na afya yangu kuendelea kuwa
mbaya. Nilitegemea nitapata nafuu nilivyoingia humu nikajua nitapona taratibu
laikini siku zilivyokuwa zinazidi kwenda najiona hali yangu inakuwa si nzuri
kwani nilikuwa nasumbuliwa na maumivu ya mgongo na kiuno hasa nyakati za usiku
nikaona vema niage mashindano nikapate mtibabu zaidi ingawa nilitamani niwepo
mpaka mwisho. Washiriki waliobaki kwa kweli nawaomba wamtangulize Mungu kwani
hakuna jambo lisilowezekana mbele ya Mwenyezi Mungu na wadumishe amani, upendo
kati yao na wapeane mambo mazuri ya kielimu ili iwasaidie wao na jamii kwa
ujumla’. Anna aliweza kujifunza mambo mbalimbali kutokana na ushirki wake kwa
wiki moja ikiwemo masuala ya kijinsia, sheria na haki za wanawake hasa umiliki wa
ardhi ambao bado ni changamoto kwa wanawake wengi. Vile vile jamii inayomzunguka
itafaidika na stadi alizopata za kutengeneza sabuni, mafuta ya mgando, bustani
ndogo ndogo nyumbani na utunzaji wa mazingira.
Mgongano kijijini
Tofauti ilitokea
baina ya wanakijiji ambapo mama shujaa mmoja alidai kuwa baadhi ya wanakijiji
wenzake wanamsema vibaya hivyo kuripoti katika uongozi wa kijiji. Viongozi hao
walichukua jukumu la kuwaita wale wote waliohusika na kuomba msamaha kwa mama
huyo kwa kile walichokifanya. Zoezi hili liliambatana na mama shujaa aliyesemwa
vibaya na wenzake kukabidhiwa mfano wa mtoto mdogo kama ishara ya kumaliza
tofauti zao ili waweze kuendelea na maisha kama kawaida. Hivi ndivyo wanakijiji
wa Maisha Plus wanavyoishi kwa amani, upndo na bila kuwekeana kinyongo
kuendeleza ugomvi ndani ya kijiji.
Mabadiliko ya Tabia nchi
Mabadiliko ya
tabia nchi ni moja ya mada zilizotolewa kwa washiriki wa muhula wa nne wa
Maisha Plus. Mada hii ilitolewa na wawakilishi kutoka Ekama Development akiwemo
Roselyn Kaihula na Hilda Mashauri. Ekana Development ni shirika lisilo la
kiserikali lililojikita katika kuwajengea uwezo wanajamii kupitia utafiti hususan
katika masuala ya haki za wanawake na watoto chini ya umri wa miaka 18.
Mwakilishi
kutoka Ekama Development Hilda Mashauri alitoa maelezo na kusema Ekama
Development hushirikiana na Oxfam katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa,
usawa wa kijinsia na kilimo rafiki kinachozingatia hali ya eneo husika ili
kuleta tija kwa mkulima. Alisema wamejiandaa vema kuendesha mashindano kwa
kuwauliza maswali washiriki wa Maisha Plus na Mama Shujaa ambapo tayari timu
mbili zimeshaundwa kwa mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumanne wiki
ijayo. Timu hizo ni Mandela na Mwalimu Nyerere. Zawadi zitatolewa kwa mshindi wa
shindano hilo ingawa aina ya zawaida haukutajwa na kubaki kuwa siri mpaka siku
hiyo ya makabidhiano kama ilivyopangwa na waandaaji wa shindano hilo. Pia
alisifu kinamama Shujaa kwa umahiri wao kueleza kilimo rafiki na namna gani
wanavyotumia kilimo hicho katika maeneo yao.
Msemaji wa timu
ya Mandela Ally Thabit alisema tumejitayarisha kuwa washindi kwani
tumeshajipanga vema na kuteua viongozi ambao watakao tuongoza na kuhakikisha
tunaibuka na ushindi siku ya Jumanne. Vile vile wakina mama Shujaa nao hawapo
nyuma wanatushirikisha na kutupa uzoefu waliokuwa nao katika masuala ya kilimo
kwenye maeneo yao ili kujidhatiti vizuri zaidi katika kuyajibu maswali
tutakayoulizwa siku hiyo ya mashindano.
Naye msemaji wa
timu ya Mwalimu Nyerere Bakari Khalid alisema hakuna sababu ya kushindwa kuwa
mshindi siku ya Jumanne kwa kuwa maswali yanayoulizwa yanatokana na kile
tulichojifunza na pia tumepewa kitini kinachozungumzia zaidi masuala ya mabadiliko
ya tabia nchi na kilimo rafiki. Pia naamini kupitia kipindi hiki jamii ya
kitanzania itakuwa imejifunza mabadiliko ya tabia nchi ni nini na namna kilimo
rafiki kinavyoweza kumnufaisha mkulima na jamii kwa ujumla wakati huo huo
unalinda mazingira.
Posted by Editor
on 11:15.
Filed under
entertainmentnews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0