Share this Post

dailyvideo

PICHA: VAENI MAVAZI HAYA YA KIAFRIKA KWENYE HARUSI ZENU.

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Nimekuwa nikichunguza sana katika Sherehe mbalimbali hasa hizi za Harusi, ambapo huanza kwa kuagwa kwa Binti na Baadae kuwa na Harusi yenyewe, kwa kweli Vijana wanajitahidi sana kutokelezea ki Afrika zaidi siku hizi za karibuni kwa kuvaa nguo ambazo asili yake ni ya hapa hapa Afrika, lakini Pia Mabinti hujitahidi sana kuvaa nguo za Kiafrika hasa wakati wa Kitchen Party pale wanapo wafunda . 

Lakini tatizo linakuja sasa wakati wa Harusi kila mtu anataka kuvaa nguo kama wazungu na kusahau kwamba kuna hizi za Kiafrika ambazo pengine wangevaa zaidi wangependeza zaidi kwa sababu zinaelezea u Afrika kabisa na kuvutia zaidi.

Zifuatazo ni Picha ambazo zinaonesha Dhahili jinsi ambavyo utapendeza katika Harusi yeko endapo utavalia ki Afrika zaidi 
Tazama kwa umakini Bibi na Bwana walivyo pendeza Wamevalia Nguo za kawaida kabisa lakini zenye kiwango cha juu, ukiwatazama hawa wameongezeka uzuri zaidi ni kutokana na haya mavazi yao
 Huu ni ubunifu wa Hali ya Juu tazama Nguo ya Kiafrika ikiwa imefanana kabisa na ua ambalo amebeba
 Wewe unaesoma hii sasa hivi hii kitu hebu tazama kwanza .. na haujaoa wala kuolewa unangoja nini sasa? hawa jamaa wamependeza sana na mavazi yao ambayo yamebuniwa ki Afrika zaidi
 

Posted by Editor on 13:55. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for PICHA: VAENI MAVAZI HAYA YA KIAFRIKA KWENYE HARUSI ZENU.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery