Share this Post

dailyvideo

TGNP WATEMBELEA KIJIJI CHA MAISHA PLUS NA KUTOA ELIMU JUU YA JINSIA KWA MAMA SHUJAA WA CHAKULA NA VIJANA WA MAISHA PLUS.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Pilika pilika za hapa na pale zilionekana katika kijiji cha Maisha Plus ambapo wanakijiji walionekana wakishughulisha na shughuli binafsi za kifamilia, kubadilishana mawazo na uzoefu walionao
 Wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus wakifuatilia Mada kwa makini wakati ikiwasilishwa na TGNP
 Pia waliweza kupata darasa kutoka kwa wawezeshaji wa masuala ya kijinsia nchini wa Mtandao wa Jinsia Tanzania. Lengo la darasa hili ni kuwawezesha washiriki wa Maisha Plus vijana na mama shujaa wa chakula kutambua na kuelewa masuala ya kijinsia kwenye shughuli zao za kazi wanazozifanya kwani washiriki wanatoka sehemu mbalimbali na wanajishughulisha na kazi tafauti ambazo zinatofautiana wengine ni wasanii, waandishi wa habari, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali, wengine bado ni wanafunzi wanaendelea na masoma
 Bakari Kharid aliyesimama Mshiriki wa Maisha Plus Kutoka Mkoa wa Shinyanga Nchini Tanzania akiwasilisha Mada
 Tunajua kwamba wakipata masuala muhimu ya kutetea usawa wa kijinsia na wanayaelewa huko wanapofanya kazi zao baadaye watayatumia vizuri sana na wataweza kuleta mabadiliko katika nchi yetu ndiyo maana tumeshiriki kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo kwenye kampeni ya ‘Haki ya Kiuchumi: Rasilimali Ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni’ alisema Deogratius Temba, Afisa Habari wa TGNP Mtandao.
 Deogratius Temba kutoka TGNP akiwasilisha mada na kutoa mafunzo juu ya Jinsia
Aliendelea na kusema kuwa tumefurahi sana kuwepo na mjadala huu mpana kupitia picha chokozi na kuona ni fursa pekee kuendelea kusambaza kampeni ya Haki ya Uchumi kwa jamii nzima mjini na huko vijijini kwasababu watu walio vijijini ni wengi  na watakapoenda kule wataendeleza hii kampeni na lubadilisha jamii yetu ya kitanzania.
 Mmoja wa Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula akitoa maoni wakati wa semina hiyo ya Jinsia katika Kijiji cha Maisha Plus
 Suala la na mfumo dume na umiliki wa ardhi limejitokeza wakatii wa majadiliano kwani mfumo dume na umiliki wa uchumi vinashirikiana kwamba kama kuna mfumo dume mwanamke na kijana hawawezi kumiliki uchumi hivyo kuendelea  kubeba mzigo mkuwa wa kulea familia.
 Wanakijiji wakifuatilia Mjadala kwa umakini
Wanakijiji wa Maisha Plus walifurahishwa na mjadala huu kwani una nia ya kumkomboa mwanamke kutokana na yale majukumu mazito anayokuwanayo nyumbani na jamii nzima inayomzunguka na kuwa na haki ya kumiliki ardhi na siyo kuwa mzalishaji pekee kama ilivyo sasa katika jamii nyingi hapa nchini. Vile vile wameweza kuona umuhimu wa kuhudhuria vikao vya kijiji ambapo wanaweza kupata fursa ya kutoa maoni na kushiriki moja kwa moja katika mchakato wa bajeti ya serikali kupitia serikali ya mtaa ambapo wengi wao hawakuwa na ufahamu huo.
Mama shujaa pia walitoa uzoefu wao kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii wanazotoka na kusema kuwa umiliki wa ardhi kwa kinamama bado ni changamoto kwani wengi wao wamebaki kuwa wazalishaji tu na kutumia ile ardhi na siyo kumiliki jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za kinamama katika kujikomboa kiuchumi. Vile vile walipongeza waandaaji kwa kuwa na mpango wa kutoa mafunzo mbalimbali yatakayowasaidia washiriki katika sehemu walizotoka na jamii kwa ujumla.
 MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA

Posted by Editor on 12:24. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for TGNP WATEMBELEA KIJIJI CHA MAISHA PLUS NA KUTOA ELIMU JUU YA JINSIA KWA MAMA SHUJAA WA CHAKULA NA VIJANA WA MAISHA PLUS.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery