Ujerumani yazindua kikosi cha mwanzo cha Kombe la Dunia
Löw amesema kuwa hana wasiwasi yoyote kuhusiana na kila mmoja wa wachezaji waliochaguliwa. Gomez ambaye ana magoli 25 katika mechi 59 alizoichezea Ujerumani, amekosa nafasi kutokana na jeraha lagoti lake la kushoto, baada ya msimu uliokumbwa na majeraha katika klabu ya Fiorentina nchini Italia.

Löw amemwita kikosini Sami Khedira kiungo wa Real Madrid ambaye hajaichezea klabu hiyo tangu mwezi Novemba mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti. Bayern imechangia wachezaji saba, Borussia Dortmund imewatoa wachezaji sita wakati Arsenal ya Uingereza ikiwatoa wachezaji watatu.
Kocha huyo ana hadi Mei 13 kuwasilisha kwa FIFA orodha yake ya mwisho isiyozidi wachezaji 30, huku muda wa mwisho wa kuwasilisha kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ukiwa Juni 2. Na kutokana na fainali ya kombe la Shirikisho la Soka la Ujerumani – DFB kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmumd, itakayochezwa mjini Berlin Mei 17, Löw amekitaja kikosi tofauti cha wachezaji 18 kitakachocheza mchuano wa kirafiki Jumanne wiki ijayo dhidi ya Poland mjini Hamburg.
Kikosi cha mwanzo
Walinda lango: Manuel Neuer, Roman Weidenfeller, Ron–Robert Zieler
Defenders: Jerome Boateng, Erik Durm, Kevin Grosskreutz, Benedikt Höwedes, Mats Hummels, Marcell Jansen, Philipp Lahm, Per Mertesacker, Shkodran Mustafi, Marcel Schmelzer
Viungo: Lars Bender, Julian Draxler, Matthias Ginter, Leon Goretzka, Mario Götze, Andre Hahn, Sami Khedira, Toni Kroos, Max Meyer, Thomas Müller, Mesut Özil, Lukas Podolski, Marco Reus, Andre Schürrle, Bastian Schweinsteiger
Washambuliaji: Miroslav Klose, Kevin Volland
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu
DW SWAHILI
