Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Kenya
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Kiasi ya watu ishirini waliuawa siku ya Jumapili katika eneo la Wajir
kaskazini mashariki mwa Kenya kufuatia mapigano makali kati ya makabila
hasimu katika eneo hilo linalopakana na Somalia.
Kulingana na umoja wa Mataifa, kiasi ya watu 75,000 wameyatoroka makaazi
yao katika miji ya Wajir na Mandera huku wengine 60,000 wakiathirika na
mapigano hayo ya kikabila. Hapo jana viongozi wa kutoka eneo hilo
walikutana na rais Uhuru Kenyatta kuzungumzia hali hiyo. Caro Robi
amezungumza na mmoja wa washiriki wa mazungumzo hayo ya kutafuta amani
Ugas Sheikh na kwanza ametaka kujua iwapo hali ya utulivu imerejea
katika eneo hilo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za
masikioni hapo chini.
Mhariri: Caro Robi
Mwandishi: Mohammed AbdulRahman
Mhariri: Caro Robi
Mwandishi: Mohammed AbdulRahman
Sauti na Vidio Kuhusu Mada

