Qatar yatafakari kwenda Mahakamani kutetea uwenyeji wa Kombe la dunia QATAR2022
Maafisa wa Qatar wanaaminika
kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na tishio la kupokonywa
uenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa Qatar 2022 kufuatia tuhuma za
rushwa .
Kamati andalizi ya michezo hiyo sasa inaaminika
kupania kufanya kila iwezalo ikiwemo kufuata mkondo wa kisheria, ikiwa
kura ya kuchagua mwandalizi wa kombe la dunia 2022,itarudiwa.
Shutuma za ufisadi katika mchakato
wa kupiga kura ya uwenyeji zilisababisha kuitishwa kwa kura nyingine
ikiwa hila itaonekana kuwa ilifanyika.

Rais wa Fifa akwepa maswali kuhusu hongo katika uteuzi wa Qatar 2022
Qatar inakana shutma za hongo.
Hata hivyo hatma yake imo mikononi mwa mchunguzi wa FIFA,Michael Garcia.
Mwanasheria huyo kutoka Marekani anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake itimiapo Juni 9.

Pauni bilioni 23 zimetumika tayari nchini Qatar
Rais wa Uefa, Michel Platini, aliyeipigia kura
Qatari, alisema kuwa atakubali kufanyike kura ya marudio iwapo shutma za
ufisadi dhidi ya Qatari zitathibitishwa.
Msimamo wake uko sawa na ule wa makamu wa rais
wa Fifa, Jim Boyce aliyesema kuwa hatakuwa na shida yoyote ikiwa
‘makubaliano yatakuwa ni kura ya marudio kufanywa.’
Maafisa wa Qatari wanadai kuwa mtaji wa takriban
pauni bilioni 23, mahsusi kwa ajili ya kombe la dunia la 2022,
itapotelea mbali iwapo Fifa italipokonya taifa hilo la ghuba haki ya
kuandaa michezo hiyo.