Wasio na makao waandamana Brazil
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Maelfu waandamana kupinga kombe la dunia
Maelfu ya wenyeji wasio na makao
mjini Sao Paolo waliandamana nje ya uwanja utakaoandaa mechi ya kwanza
ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga gharama ya juu ya mashindano
hayo.
Maandamano hayo yaliwadia siku moja tu baada ya
rais wa Brazil Dilma Rousseff kuwahakikishia wageni na mashabiki wa
kandanda kuwa kamwe hatoruhusu maandamano yatie doa kwenye kipute hicho
cha kombe la dunia.

Maelfu waandamana kupinga kombe la dunia
Takriban waandamanaji 10,000
waliziba barabara zote mjini Sao Paolo wakiishinikiza serikali ya bi
Rousseff iwekeze katika sekta ya afya elimu na ipunguze gharama ya juu
ya usafiri wa umma.
Zaidi ya watu milioni moja waliandamana katika
barabara za miji yote ya Brazil wakishinikiza serikali kupunguza
ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake kwa maandalizi ya kombe
la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.

10,000 Waandamana kupinga Kombe la Dunia
Licha ya hakikisho la rais Rousseff wafanyikazi
wa reli walitishia kuanza mgomo upya huku polisi wa trafiki mjini Sao
Paolo pia wakitishia kuanza mgomo Alhamisi.
Mapema wiki hii serikali iliwaongezea polisi
wote mshahara ilikuzuia mgomo uliotishia kuporomosha hali ya utengamano
huku fainali ya kombe la dunia likinukia.
Serikali imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano wakati wa kombe la dunia.
BBC SWAHILI

Posted by Editor
on 12:14.
Filed under
sportnews
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0