Share this Post

dailyvideo

Onyo la China kuhusu Hong Kong

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399China yaonya mataifa ya kigeni kutoingilia maswala ya Hong Kong

Uchina imesema kuwa haitawavumilia wahaini kutoka nje ya nchi wanaounga mkono maandamano yasiyo halali nchini humo.
Kundi lijulikanalo kama Occupy Central ndilo linalolengwa kwa sababu limekuwa likiunga mkono juhudi za maandamano ya maelfu ya watu wanaounga mkono kuimraishwa kwa Demokrasia nchini Uchina.
Katika kile kinachoaminika kulenga maandamano yanayoendelea katika jimbo la Hong Kon, Uchina inaonya mataifa mengine yasijiingize kwa kila inachoamini na maswala ya ndani ya Uchina.
Uchina mara kwa mara hutoa onyo kwa mataifa mengine yasijiingize katika jimbo hilo lake linalotaka kuendesha mambo yake kivyake.

Serikali ya China inaamini kuwa Hong Kong Inauwezo wa kukabiliana na maandamano

Mapema mwezi huu Uchina iliudhika sana na matamshi ya Chris Patten, aliyekuwa wakati mmoja Gavana wa Hong Kong, aliposema kwamba Uingereza ina wajibu wa kutoa taarifa kwa niaba ya wakazi wa Hong Kong, eneo lililokuwa koloni yake wakati mmoja.
Baraza Kuu la Kitaifa la Uchina, ambalo ni kiungo muhimu katika Serikali, limesema kuwa lina imani kwamba Serikali ya Jimbo la Hong Kong, ina uwezo wa kukabiliana na maandamano hayo kibinafsi bila kuingiliwa na yeyote.
Kuna hofu kuu Hong Kong kuwa huenda Serikali Kuu ikatumia polisi wenye silaha kuzima maandamano hayo.

BBC

Posted by Editor on 14:43. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Onyo la China kuhusu Hong Kong

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery