Share this Post

dailyvideo

MAMBO YAHARIBIKA BURKINA FASO JESHI LAPINDUA NCHI


Bunge la Burkina Faso limetekezwa moto

Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa. Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore. Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Mmoja wa wabunge nchini Burkina Faso akitorokea kuokoa maisha yake.
Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27. Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .
Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji. Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa. Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Uharibifu katika majengo ya serikali Ougadougou
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena. - BBC

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Posted by Editor on 13:23. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAMBO YAHARIBIKA BURKINA FASO JESHI LAPINDUA NCHI

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery