MKEMIA: MKOJO WA MASOGANGE UMEBAINIKA KUWA NA HEROIN
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Mkemia
kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima, ameiambia
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa sampuli ya mkojo wa msanii Agnes
Gerald maarufu kama Deal ama Masogange (28) umebainika kuwa na dawa ya
kulevya aina ya heroin.
Akitoa
ushahidi leo Jumatano mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri,
shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mashtaka, akiongozwa na Wakili wa
Serikali, Constantine Kakula, ameiambia mahakama kuwa mnamo February 15,
2017 askari wawili kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Koplo Sospeter na
WP Judith, walimfikisha Masogange ofisini kwake kwa lengo la kumfanyia
vipimo vya mjono wake.
Alisema
baada ya kuwapokea, alimsajili Masogange na kumpa namba ya mahabara 446
/2017 na kisha kuwakabidhi kifaa maalum kwa ajili ya kuweka sampuli ya
mkojo.
Alidai
baada ya kupokea sampuli ya mkojo ya Masogange alifanyia uchunguzi kwa
kutumia kemikali na kubaini kuwa mkojo wake una chembechembe za dawa za
kulevya aina ya heroin ambazo kwa kitaalamu zinajulikana kama Diacety
Imophine.
Aidha, alisema uchunguzi zaidi ulibaini chembechembe za dawa nyingine ya kulevya aina ya Oxazepam.
Shahidi
huyo alidai baada ya kufanya uchunguzi huo, aliandaa taarifa ya
uchunguzi kuhusiana na sampuli hiyo ya mkojo ambapo aliisaini yeye
mwenyewe na kuthibitishwa na kaimu mkemia mkuu wa serikali.
Shahidi huyo alimtambua Masogange kwa ndiye aliyepelekwa kuchukuliwa sampuli hiyo ya mkojo ofisini kwake
Posted by Editor
on 10:58.
Filed under
entertainmentnews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0