Share this Post

dailyvideo

Dogo Janja kurudi kesho Dar kwa ndege kusaini mkataba mnono



Waswahili wanasema wakati wewe unasema cha nini, wengine wanajiuliza watakipata lini? Wakati story za Tip Top Connection kuzinguana na Dogo Janja zinaanza kupungua pole pole kwenye midomo  ya watu, magazeti na kwenye radio, kumeibuka good news kwa mashabiki wake.

Mpaka unasoma story hii ni kwamba kesho kijana anapanda ndege kurudi Dar es Salaam baada ya kupigiwa simu na mtu ambaye ameahidi kumsaidia kimuziki na kumsomesha pia.

Akiongea na East Africa Radio mchana huu, dogo huyo amesema anakuja kuuangalia mkataba huo kama ukimridhisha basi atasaini na mambo yaendelee.

Tayari anasema amepata baraka kutoka kwa wazazi wake.

Amewaomba mashabiki wake wampokee airport ili kushow love!

Kila lakheri Dogo Janja.
Source: Leo Tainment 

Posted by Editor on 16:04. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Dogo Janja kurudi kesho Dar kwa ndege kusaini mkataba mnono

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery