Share this Post

dailyvideo

Wakili Wa Kujitegemea na Mwenyekiti wa UVCCM Emmanuel Makene Azungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mgomo Wa Madaktari Nchini


Emmanuel Makene,Wakili wa kujitegemea na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni.
---
Miaka
48 iliyopita, Raisi wa Tanganyika wakati huo, Mwl. Julius Kambarage
Nyerere na Raisi wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani
Karume; walisaini mkataba ulioitwa Mkataba wa Muungano (Articles of
Union) kwa ajili ya kuunganisha nchi zao (Zanzibar & Tanganyika)
kuwa nchi moja yenye dola moja.


Mkataba
huo ulikuwa mkataba wa Kimataifa (International Treaty) na kila nchi
ilipaswa kuridhia mkataba huo katika sheria za nchi husika. Kazi ya
kuridhia ni kazi ya Bunge la kila nchi.


Kwa
upande wa Tanganyika, tarehe 25 April, 1964, Bunge la Tanganyika
liliridhia Mkataba wa Muungano na Bunge la Tanganyika likatunga sheria
iliyoitwa Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Namba 22 ya
mwaka 1964. Hii ina maanisha kuwa mkataba wa Muungano ni sehemu ya
sheria za nchi (Tanganyika) kuanzia tarehe 26 Aprili 1964.


Kwa
upande wa Zanzibar, wao hawakuwa na Bunge wala Baraza lolote la
Wawakilishi. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar ndio lilikuwa likifanya
kazi kama Bunge la Zanzibar na Baraza la Mawaziri. Hivyo Mkataba wa
Muungano uliridhiwa na kupitishwa na Baraza la Mapinduzi. Isipokuwa
kutokana na uzembe au kutokuwa makini kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
tangazo la kuridhia Mkataba wa Muungano haukutolewa katika Gazeti la
Serikali (Government Gazette) la Zanzibar. Hivyo Mkataba wa Muungano
ulipitishwa na kuthibitishwa na Baraza la Mapinduzi.Kusoma Zaidi Bofya na Endeleaa>>>>>>

Posted by Editor on 19:14. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Wakili Wa Kujitegemea na Mwenyekiti wa UVCCM Emmanuel Makene Azungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mgomo Wa Madaktari Nchini

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery