Warembo wa 5, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvis Majaji, wakati wa shindano hilo.
Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.
Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, Majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall........
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Geneviv Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.
Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders, ambapo pia wadhamini wengine ni pamoja na mtandano huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Kampuni ya SPM:- Sufiani Photo Magic, Redd'd, Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, B-Ze Hotel, Clouds Fm, Endepa, Gazeti la Jambo Leo na Simple & Easy Car.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.....
Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.
Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea..........
Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Sax phone kabla ya kuanza kwa shindano hilo...
Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.
Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora ...............
Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Sax Phone......
Gavana Ndullu akibonyesha kitufe cha Komputya kuashiria uzinduzi rasmi wa mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana na hati fungani kwa njia ya mtandano (online) kwenye mnada. (Picha ma Tiganya Vincent wa Maelezo –Dar es Salaam).
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndullu akizundua rasmi mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana za Serikali na hati fungani kwa njia ya mtandano(online) kwenye mnada na hivyo kupunguza ule utaratibu wa dhamana wa kupeleka karatasi katika Benki ili kupata huduma hiyo.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndullu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana za Serikali na hati fungani kwa njia ya mtandano (online) kwenye mnada na hivyo kupunguza utaratibu wa dhamana wa kupeleka karatasi katika Benki ili kupata huduma hiyo.
Profesa Ndullu (kushoto) na Naibu Gavana wa BoT Dkt Natu Mwamba (kulia) wakinukuu maswali mbalimbali ya waandishi wa jijini Dar es salaam kabla hawajaanza kuyatolea ufafanuzi.
Msajili wa Bodi ya wahandisi nchini Mhandisi Steven Mlote akijibu maswali ya waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Prof. Ninatubu Lema.
Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa wahandisi nchini Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya 10 ya jumuia ya wahandisi kuanzia tarehe 6-7 mwezi wa tisa mwaka huu. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kulia ni Msajili wa Bodi Mhandisi Steven Mlote.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
|
TOP 5 ya vipaji Miss Ilala, kutoka kushoto ni Merry Chizi, Stella Morris, Amina Sangawe, Magdalena Munisi na Mectilda Martin baada ya kutangazwa washindi jana Nyumbani Lounge. |
|
Majaji kazini |
Amina Sangawe akirusha kete yake kwa majaji
Wadau wa Urembo kutoka Ukonga nao walikuwepo
|
Benny Kisaka na Rutta kushoto |
|
Majaji wetu, asante kwa kazi nzuri |
|
Epraim Kibonde na mnazi mwenzake wa Simba, Philipo |
Mrembo akionesha kipaji cha kuchora
|
Kazi ya mapacha ndio hii |
|
Mapacha jukwaani |
|
Ubora wa kazi ni tofauti na umaarufu wa jina...Cheki Mapacha, utafikiri bendi gani sijui la DRC lenye maskani yake Ufaransa |
|
Warembo wakifuatilia shindano hilo, niwarembo wa miaka ya nyuma Ilala na Kinondoni |
|
Mapacha habari nyingine bwana |
|
Mtangazaji mpya wa Times FM 100.5 Gadan G, ukipenda muite Kapteni au Baba Some Food akiwa na asali wake wa moyo...Lady Jidee. upande wangu huku ni Lisa |
VIMWANA watano usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kuingia fainali ya kuwania taji la mrembo mwenye kipaji zaidi katika shindano la Miss Ilala 2012, lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam.
Vimwana hao ni Merry Chizi, Stella Morris, Amina Sangawe, Magdalena Munisi na Mectilda Martin, ambao waliwapiku wasichana wenzao wengine wanane, Suzan Deodatus, Whitness Michael, na Elizaberth Pertty, Wilmina Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Noela Michael na Phillios Lemi.
Mshindi wa taji hilo, atatajwa katika kilele cha shindano la Miss Ilala 2012 kwenye ukumbi huo huo, Septemba 7, mwaka huu.
Shindano hilo lililoanza saa 2;00 usiku, lilipambwa na burudani ya bendi ya mapacha watatu na mastaa kibao wa bongo walikuwepo.
Warembo hao, wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi, Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na Dickson Daudi wa THT katika shoo.
Miss Ilala, yenye rekodi ya kutoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na Salha Israel anayeshikilia taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake nzuri mwaka huu.
Miss Ilala inahusisha warembo kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga.
SOURCE: http://bongostaz.blogspot.com/