CHADEMA KUMFIKISHA MAHAKAMANI NAPE NNAUYE
Mbunge
wa Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika akizungumza na waandishi
wa habari leo asubuhi. (Picha na Habari Mseto Blog)
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
kufuatia madai ya uzushi na uongo aliyoyatoa tarehe 12 Agosti 2012 kuwa
anao ushahidi kwamba CHADEMA kimekuwa kikiwahadaa wananchi kwa
kuwachangisha fedha huku kikipokea mabilioni ya fedha kutoka kwa
wafadhili kutoka nje.
Izingatiwe
kuwa matamshi yake yalitangazwa na vyombo vya habari vya kielekroniki
ikiwemo vituo vya televisheni, radio na kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii tarehe 12 Agosti 2012 na katika kurasa za mbele za magazeti
mbalimbali tarehe 13 Agosti 2012.
Bodi
ya Wadhamini wa CHADEMA iliagiza wanasheria wamwandikie barua ya
kumtaka kukiomba radhi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kutumia
njia ile ile aliyotumia kufanya propaganda chafu za kuikashifu na
kuifitisha CHADEMA kwa umma wa watanzania ikiwemo kuzusha kuwa upo
uwezekano wa CHADEMA kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya
kuiweka nchi rehani.
Tayari
ameshaandikiwa barua ya kisheria tarehe 24 Agosti 2012 ya kumtaka aombe
radhi na kulipa fidia ya bilioni tatu kwa matamshi hayo ya uzushi na
uongo yenye maana ya kuwapotosha waliyoyasikia na kuyasoma kuwa CHADEMA
kinawalaghai wananchi, kina viongozi wasio waaminifu na kwamba kiko
tayari kuuza nchi wa uroho wa madaraka.
Kipaumbele
cha CHADEMA katika suala hili ni kuombwa radhi hata hivyo kiwango cha
fidia ya fedha kwa fedheha kilichotakiwa ni fundisho kuwa uzushi na
uongo unagharimu.
Ikumbukwe
kwamba tarehe 12 Agosti 2012 nilitoa kauli ya awali baada ya mkutano
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na waandishi wa habari ambapo pamoja
na mambo mengine nilieleza kwamba tutatoa tamko la kueleza hatua za
ziada baada ya kupata taarifa kamili aliyoitoa.
Katika
kauli hiyo nilitoa mwito kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete
kueleza watanzania iwapo propaganda hizo chafu zina baraka zake; hivyo
ukimya wake mpaka sasa kuhusu matamshi hayo inakifanya CHADEMA kuwa na
imani yenye shaka (benefit of doubt) kwamba Nape hakutumwa na chama
chake kutoa matamshi aliyoyatoa.
CHADEMA
inachukua fursa hii kuutaarifu umma kwamba asipotekeleza matakwa hayo
ndani ya siku saba kuanzia tarehe hiyo aliyopokea barua hatua nyingine
ya kumfikisha mahakama kuu zitaanzishwa ili aweze kuchukuliwa hatua
zaidi.
Pamoja
na kuchukua hatua za kisheria, CHADEMA kinaendelea kutimiza dhima yake
ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni
thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa pamoja na mikakati
mingine kutekeleza operesheni ya vuguvugu la mabadiliko nchini (M4C) na
tunawashukuru wananchi kwa kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kwa hali
na mali katika maeneo mbalimbali nchini.
Imetolewa Tarehe 26 Agosti 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Posted by Editor
on 13:03.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0