Fahamu Tabia za wanyama Dume na maisha yao
Simba hulinda Familia yake
Wanyama Dume hujihami kwa jambo lolote
Mara wapatapo nafasi wanyama Dume hucheza na watoto wao
Wanyama Dume kwa pamoja huwa na ushirikiano wa hali ya juu
Wanapo kutana wanyama dume huwa na mambo mbali mbali
Watoto wanyama, Mara nyingi hupenda kuwalalia wanyama hao na kuwa nao karibu
Wanyama dume huakikisha kwamba watoto wao hawapati shida
Wanyama hawa hufurahi kwa pamoja
Mtoto mara anapo ona baba yake yupo jirani huweza kujiachia
Mnyama huyu ni Bonus kwenu
*****
Wiki iliyopita tulileta kwenu tabia za wanyama wa kike ambapo tuliona jinsi wanavyo penda kuishi ana watoto wao.
Leo tueona pia tuwaletee maisha ya wanyama wa kiume yaani madume, wanyama hawa ambao tumeweka tofauti tofauti kila mmoja wao anatabia zake lakini walio wengi wanatabia zinazo lingana ama kufanana, Katika baadhi ya tabia hizo wanyama dume wengi wanapenda watoto wao sana, hupenda kucheza nao na kuwafundisha mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwafundisha kuwinda, kutafuta chakula na kula chakula, wanyama wengi madume hupenda kuona kuwa watoto wao na wanyama jike wanaishi kwa amani bila bugudha za aina yoyote ile.
Wanyama wengi wa kiume hupenda kushirikiana katika mambo mbalimbali, lakini licha ya kusaidiana huko wanyama dume hupenda kuoneshana ubabe wakati mwengine hasa wanapo taka kupata jike, atakaye shinda ndiye anaondoka na jike hilo.
Kuna baadhi ya wanyama kama Sokwe na Nyani hawa hutulia na familia zao moja kwa moja mpaka uzeeni, kama alianza kuzaa na mnyama mwenzake huyo wataendelea kufanya hivyo mpaka mwisho.
Lakini wanyama dume kama Simba,Mbwa hawa hawanaga hizo wanaweza kuwa na watoto na wakaja kuwazalisha watoto wao tena.
Haya ndiyo mambo kiasi ambayo ni muhimu ukayajua kuhusiana na wanyama Dume
imeandaliwa na
Fredy Tony Njeje
Mtaalam wa mazingira wa This Day Magazine
Posted by Editor
on 07:38.
Filed under
environmentnews,
feature,
gallery
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0