Ghasia mjini Mombasa baada ya kuuawa Aboud Rogo
Mji wa Mombasa nchini Kenya umekumbwa na vurugu kufuatia kuuawa hapo jana kwa mhubiri wa dini ya Kiislamu Aboud Rogo Mohammed, ambaye alihusishwa na makundi ya Kigaidi.
Taarifa kutoka mjini humo zinaeleza kwamba vurugu hizo zimechukua mweleko wa kidini, ambapo makanisa mawili yamevamiwa na mtu mmoja kuuawa. Muda mchache uliopita Daniel Gakuba amezungumza kwa njia ya simu na kamanda wa polisi katika mkoa wa pwani Agrey Adoli, ambaye alianza kwa kusema kuwa kile kinachoshuhudiwa sasa ni zaidi ya maombolezo kwa ajili ya mhubiri huyo.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri:Josephat Charo
Posted by Editor
on 13:44.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0