HOFU YA USHOGA YAIFANYA UGANDA KUJIPANGA DHIDI YA UHALIFU WA INTERNET.
Serikali ya Uganda imetangaza kuimarisha usalama wake wa mtandao wa internet baada ya kugundua kuwa wahalifu wamejipenyeza katika mfumo huo.
Siku kadhaa zilizopita wanaharakati wa haki za mashoga walijipenyeza katika tovuti kadhaa za serikali siku kadhaa zilizopita, ikiwemo tovuti ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Wanaharakati hao walitumia tovuti hizo kuchapisha ujumbe ambao ulielezea uungaji mkono haki za mashoga, kama vile maafisa wa serikali ndio waliouandika.
Uganda tayari imetangaza kitendo cha ushoga kuwa kinyume cha sheria, lakini mswada wenye utata ambao utafanya adhabu yake kuwa kali zaidi ndicho kilichochoea watu hao kujipenyeza katika tovuti hizo.
Mswada huo mpya awali ulitaka adhabu ya kunyongwa kwa watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ngono kwa watu wa jinsia moja.
Posted by Editor
on 13:38.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0