Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu" Wafungua Tawi Jipya la Chadema Houston Nchini Marekani
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman
Mbowe akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua tawi jipya la Chadema Houston,Tx nchini Marekani
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman
Mbowe akikabidhi Kadi kwa wanachama wapya wa Chadema nchini Marekani muda mfupi baada ya kuzindua tawi jipya la chadema Houston
Sehemu ya Umati wa Watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Chadema Houston,TX uliofanywa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman
Mbowe na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu"
Sehemu ya watoto waliojitokeza kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Chadema Houston nchini Marekani.Picha Zote na Chadema
---
*Wanachama wapya wa Chadema Houston Wamejitolea pikipiki
116 kama
mchango wao kwa Chama kwa ajili ya M4C.
*Wameahidi kuchangishana pesa ili kununua gari
litakalosaidia
katika operesheni ya M4C
Baada ya kufungua Tawi jijini Washington DC tarehe 27 MAY 2012, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefungua tawi lingine la pili tarehe 25 AUGUST 2012
jijini Houston, Texas nchini Marekani ikiwa ni muendelezo wa kufungua
matawi mbalimbali nchini humo. Sherehe hiyo ya Ufunguzi wa Tawi la
Chadema Houston imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman
Mbowe na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu". Viongozi
wengine waliohudhuria ni Katibu wa Chadema Tawi la Washington DC Mhe
Isidory Lyamuya na aliyekuwa katibu wa Kwanza wa Chadema Washington DC
Mhe Liberatus Mwang'ombe.
Sherehe hizo ambazo zilifanyika katika Hotel
ya Marriot zilihudhuriwa na Watanzania wengi waishio Houston. Katika
Sherehe hizo wanachama wengi waliamua kujivua gamba na kuvaa Gwanda kama
ishara ya kutaka kulikomboa Taifa la Tanzania linalozama katika Bahari
ya Mafisadi. Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Houston
Ndugu Fuefue ameahidi kufanya mambo makubwa kwa kushirikiana na
wanachadema wa Houston na wapenda mabadiliko wote kuchangia kwa hali na
mali katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya M4C. Viongozi hao wa
Chadema Houston wameahidi kuchangishana pesa ili kununua gari
litakalosaidia katika operesheni ya M4C. Pia wameahidi kutoa pikipiki
116 kama mchango wao kwa Chama kwa ajili ya M4C.
Posted by Editor
on 12:04.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0