Share this Post

dailyvideo

MWONGOZO KUHUSU UTARATIBU WA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI KUSHIRIKI KUTOA MAONI YAO KUHUSU UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph warioba (katikati) akiongea katika mkutano na Waandishi wa Habari hivi karibuni. Kulia ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid na Bw. Casmir Kyuki (kushoto)

Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni www.katiba.go.tz
Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
1.     1. MAMBO YA KUZINGATIA
Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:
Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.
(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:
Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tz This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ), nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769
(ii)Utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume.
(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:
Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).
Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania pekee.

Posted by Editor on 13:52. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MWONGOZO KUHUSU UTARATIBU WA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI KUSHIRIKI KUTOA MAONI YAO KUHUSU UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery