TAASISI YA KIMATAIFA YAVUTIWA NA JUHUDI ZA TANZANIA KUDHIBITI SILAHA HARAMU
Bw. Eric Berman Mkugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa inayohusika na utafiti wa masuala ya silaha ( Small Arms Survey Poject) yenye makao yake Geneva, Uswisi, akifafua jambo wakati wa uziduzi ya taarifa ya utafiti uliofanyika mwaka huu. Mkurugenzi huyo ameonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika kufanya utafiti kuhusu juhusi za Tanzania katika kudhiti silaha haramu. Amesema taasisi yake imevutiwa sana na umakini wa tanzania katika zoezi hilo.
Na Mwandishi Maalum
Taasisi inayotambuliwa na kuheshimika kimataifa kama chanzo rasmi cha utoaji taarifa zinazohusu silaha, imeelezea nia yake ya kushirikiana na Tanzania kufanya utafiti kuhusu zoezi la udhibiti wa silaha haramu.
Hayo yameelezwa na Bw. Eric Berman, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ijulikanayo kama Small Arms Survey Project yenye Makao yake Makuu Geneva, Uswisi, wakati alipokutana na kubadilishana mawazo na Meja Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa.
“ Tunafahamu Tanzania ni kati ya nchi zilizomakini kwenye utekelezaji wa zoezi la udhibiti wa silaha haramu, ikiwamo uwekaji wa alama kwenye silaha. Kwa hiyo tungependa kufanya mazungumzo ya kuangalia namna gani tunaweza kushirikiana nakufanya utafiti kuhusiana na juhudi zenu hizi” akasema Bw. Berman.
Aidha akaongeza kwamba hata wenzao kutoka Taasisi ya Kanda ya Afrika Mashariki inayohusika na masuala ya silaha ndogo ndogo ( RECSA) pia wamewadhibitishia kwamba Tanzania ni kati ya nchi makini.
Nia hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji Berman ya kutaka kushirikiana na Tanzania kufanya utafiti huo, imefuatia mchango alioutoa Meja Ibuge kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa Mkutano wa pili wa Mapitio ya Mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu silaha ndogo na nyepesi ( United Nations Program of Action).
Mkutano huo ambao ni wa wiki mbili unafanyika hapa UM, na umefunguliwa siku ya jumatatu wiki hii na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson. Madhumuni mkutano huu pamoja na mambo mengine ni kutathimini mchakato wa utekelezaji wa mpango huo ambao nchi wanachama waliupitisha kwa kauli moja mwaka 2001.
Katika mchango wake, pamoja na mambo mengine, mjumbe huyo wa Tanzania katika Mkutano huo, ameeleza kwamba Tanzania siyo tu imekuwa ikitekeleza kwa vitendo zoezi la udhibiti wa silaha haramu, lakini pia inaendelea na kazi kubwa ya uwekaji alama kwenye silaha, zinazomilikiwa na serikali na zinazomilikiwa na watu binafsi.
“ Mwaka 2009, Serikali ya Tanzania ilianza zoezi la kuweka alama kwenye silaha, hadi leo hii tayari tumeshaweka alama kwenye silaha zaidi ya 38,000 zinazomilikiwa na serikali na zinazomilikiwa na watu binafsi” akasema Meja Ibuge Na kuongeza kuwa zoezi hilo limehusisha mikoa 12 ya Tanzania Bara na kwamba ni zeozi endelevu ambalo lengo lake ni kuhusisha mikoa yote 30 nchini.
Akafafanua zaidi kwamba serikali kwa kushirikiana taasisi za kikanda kama vile RECSA na GZT imeendelea na jitihada za kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali maofisa wake.
“ Tumejidhatiti kuendelea na zoezi hili tukiamini kwamba hatimaye taasisi za kikanda na kimataifa nazo zitaendelea kuchagiza juhudi hizi pamoja na ushirikiano ili hatimaye sote kwa pamoja tufanikishe kuondokana na biashara haramu ya silaha ndogo na nyepesi” akasisitiza Ibuge.
Akizungumzia kuhusu matumizi ya silaha haramu pamoja na usambazaji wake, Meja Ibuge amesema, Tanzania inawasiwasi juu ya hali ya ongezeko la utengenezaji, uhamishaji na usambazaji haramu wa silaha hizo ikiwa ni pamoja na ulibikizaji usiodhibitiwa.
Aidha akaongeza kwamba Tanzania inamashaka na kuwapo kwa mlundikano usio wa uwiano wa mahitajio ya silaha husika kwa matumizi halali kati ya m nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Akasema ulundikaji huo wa silaha kukichangiwa na kutokuwapo kwa udhibiti wa uzagaaji wake ni tisho kubwa kwa amani, usalama na maendeleo hususani Barani Afrika.
Utafiti ambao umefanywa na Taasisi ya Small Arms Survey project umeonyesha kwamba kuna takribani silaha ndogo milioni 875 ambazo ziko kwenye mzunguko duniano kote. Silaha hizo zimetengenezwa na makampuni zaidi ya elfu moja kutoka karibu nchi100.
Aidha ripoti ya utafiti huo ambayo ni ya mwaka huu wa 2012 na imezinduliwa wakati wa Mkutano huu , imebainisha kwamba kumekuwapo na ongezeko la dhamani katika uhamishaji wa kimataifa wa silaha ndogo na nyepesi, kutoka dola 4 bilioni mwaka 2006 hadi dola 8.5 bilioni mwaka huu.
Posted by Editor
on 11:39.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0