BAADA YA KUSAINI KUKATAZA WANAWAKE WASIVAE NGUO FUPI NA ZINAZO ONESHA MANYONYO, SASA WANAUME WATAKAO KAMATWA WANAMAHUSIANO NA JINSIA MOJA KUFUNGWA MIAKA 14! - MUSEVENI
Rais
wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa
adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Rais
Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla
iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi wa
habari.
Mswada
huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14
jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza,
Adhabu
ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki
mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili
waliokubaliana kufanya hivyo.
Adhabu
hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha
watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya
Ukimwi.
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.
BBC SWAHILI