MUGABE ATIMIZA MIAKA 90
Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa
kutimiza umri wa miaka 90. Hata hivyo sherehe yake imegubikwa na
wasiwasi juu ya afya yake.
Wakati
ambapo wasaidizi wake wanasema afya yake iko vizuri, wiki hii alienda
tena nchini Singapore kwaajili ya upasuaji wa macho na hivyo kuamsha
tena wasiwasi. Bado yupo nchini humo na sherehe yake ya kuzaliwa
itafanyika uwanjani siku ya Jumapili na inadaiwa kugharimu dola milioni
1.
Kiongozi huyo wa Zimbabwe tangu mwaka 1980, amekuwa akienda Singapore kutibiwa mara kadhaa.
Mugabe alizaliwa tarehe 21 February 1924. Sherehe
yake itahudhuriwa na maelfu ya wananchi kwenye uwanja wa Marondera, mji
uliopo kilomita 75 mashariki mwa mjini mkuu, Harare.Kutakuwepo na muziki, michezo na chakula