DIAMOND PLATNUMZ AVUNJA UKIMYA NI BAADA YA NGOMA YAKE YA NUMBER ONE REMIX KUSHIKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA TRACE TV , AFRICA 10
Jana mida ya saa Tano usiku ndani ya Moja ya Tv kubwa za
Muziki Afrika iendayo kwa Jina la Trace Tv kulikuwa na African 10, yaani ngoma
10 kali sana zinazotamba Afrika kwa sasa, ambapo wale wanamuziki wakubwa wote
kama Psquare, Dovido, J Martins, wakali kutoka Afrika Kusini na mataifa mengine
toka Barani Afrika hushindanishwa hapo.
Hata Hivyo baada ya count down yote kupita ngoma ya kumi
mpaka ya tisa zilishikwa na wasanii wakali na wakubwa pekee kutoka pande
zengine za afrika na si Afrika mashariki.
Na Mwishoni kabisa mambo yalibadilika Ghafla na kushangaza
watazamaji wengi pale ambapo Ngoma ya Number One Remix yake msanii Diamond
aliyomshirikisha mkali Dovido ilivyo
pigwa na kushika nafasi ya kwanza.
Kitu ambacho kimedhihilisha ya kwamba Afrika Mashariki
Hususani Tanzania ni wakali katika Muziki, kwa maana kuna ngoma ya Dovido
ameiachia Juzi tuu inaitwa Eye ambayo kwa sasa inashika nafasi ya Tatu, huku
wakina P square wakiwa bado huko mkiani.
Kwa ujumla Kijana Diamond anastahili Pongezi za aina yake na
kwamba wanamuziki wengine wa Tanzania wanatakiwa kuiga Mfano huu kwenda 'Level
Zengine' na si kulidhika tuu kwa hapa hapa nchini.
Tazama hapa baadhi ya picha za wimbo huo hapa chini na
itazame ngoma hiyo hapa.
Endelea kuangalia chini kuona video
Picha na Habari na This Day Magazine
VIDEO
Posted by Editor
on 13:13.
Filed under
entertainmentnews,
feature,
gallery
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0