KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATUA WINDHOEK
Kikosi
cha Taifa Stars kimeondoka leo alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa
ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) dhidi ya wenyeji itakayochezwa Machi 5 mwaka huu.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu
25 unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF). Timu imefikia hoteli ya Safari jijini humo.
Mechi
hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars
kipo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana
leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF).
Namibia
(Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia
kambini jana (Machi 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi
zake zilianza kuuzwa Februari 28 mwaka huu.