MAAJABU NA KWELI TUKIO KATIKA PICHA: CHATU APAMBANA NA MAMBA KATIKA MAPIGANO MAKALI AMSHINDA NA KUMLA.
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio
hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na
kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC.
"Tulimuona
Nyoka akipambana na Mamba, alifanikiwa kumpinda mamba na kumzunguka
hasa katika sehemu ya miguu yake ili kumdhibiti.''
"pambano
lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake
juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kunza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua Nyoka dakika kumi na tano kuma yule Mamba.
''Bila
shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatuui alikokwenda, baada ya mlo
wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu
mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa
wanyama hao wawili walipambana kwa karibu masaa 5. Hatimaye wote
walionekana kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce
BBC