STORY: WAPAMBE WAMFUATA VICKY KAMATA WODINI
Stori: Waandishi Wetu
MAMBO yanazidi
kuwa mambo kuhusu ile ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyoyeyuka katika
dakika za majeruhi, safari hii Risasi Mchanganyiko limefanikiwa kuwanasa
baadhi ya wapambe ambao walitakiwa kuwa kwenye msafara wa harusi hiyo
kutoka kanisani hadi ukumbini.
Wapambe
hao walitia timu kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Vicky katika Hospitali
ya General iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita
(ambayo ndiyo ilikuwa ndoa ifungwe).
WAPAMBE WATATU
Katika
idadi ya watu sita waliofika kumjulia hali Vicky, watatu wakiwemo
wanaume wawili ndiyo waliokuwa wamevaa sare ya harusi hiyo ambayo
ingetawaliwa na rangi ya purple ‘papo’ (angalia picha ukurasa wa mbele).
SARE KAMILI
Iilithibitika
kwamba sare za shughuli hiyo zilishashonwa, wanaume waliokuwa mstari wa
kusindikiza maharusi walitakiwa kuvaa suti nyeusi (single button),
shati jeupe na tai fupi (necktie) yenye rangi ya papo.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, wanawake ambao pia walikuwa kwenye msafara wa
maharusi (ma-maids) walitakiwa kuvaa magauni ya rangi hiyohiyo ya papo.
KWA NINI WALIVAA HUKU WAKIJUA HARUSI HAIPO?
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, wapambe hao walikuwa ndani ya mavazi hayo kwa
sababu walijua baada ya ndoa kuyeyuka, wasingeweza kuvaa siku nyingine.
“Unajua
wale si kwamba walikwenda pale na sare wakijua ndoa ipo, walijua kabisa
kwamba haipo ila sasa kwa sababu ndiyo ilikuwa siku yenyewe ilibidi
wajipigilie tu kama kusafisha hali ya hewa au wengine husema ‘kuoshea’
jina,” kilisema chanzo.
UKUMBI WADODA
Waandishi
wetu Jumapili iliyopita walikwenda mbele zaidi kwa kufika kwenye
Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam ambako
shughuli ya ndoa hiyo ingefanyikia.
Mfanyakazi
mmoja ambaye aligoma kutaja jina kwa sababu si msemaji wa hoteli hiyo
alisema ukumbi ambao ulikuwa utumike kwa harusi ya Vicky Kamata uitwao
Kili Marquee ulilala doro baada ya wahusika kuweka wazi kwamba hakuna
harusi tena.
“Ukumbi ulilala mtupu, taarifa zilishakuja mapema kwamba hakuna harusi,” alisema mfanyakazi huyo.
Alipoulizwa ni kwa nini wasikodishe kwa mtu mwingine, mfanyakazi huyo alisema si utaratibu wa hoteli hiyo.
“Wale
walishalipia, sasa ukisema ukodishe kwa wengine kwa sababu harusi haipo,
je, ingetokea harusi ikaja ghafla na kukuta wateja wengine? Si ingekula
kwetu?” Alisema mfanyakazi huyo.
MILIONI 40 ZA MCHANGO ZATATIZA
Kuna habari kwamba, zaidi ya shilingi milioni arobaini ambazo zilikuwa za mchango wa harusi hiyo zimetoweka kusikojulikana.
Fedha
hizo zilichangwa na wadau mbalimbali katika kufikia kile kiasi cha
shilingi milioni 96 ambazo zilidaiwa tangu awali kwamba ndizo
zingefanikisha shughuli nzima ya harusi hiyo iliyotarajiwa kuwa ya
kifahari.
Vicky
Kamata akiwa katika pozi na mwanaume aliyepanga kuoana naye
anayejulikana kwa jina la Charles ambaye kwa sasa hajulikani alipo.
BWANA HARUSI HAJULIKANI ALIPO
Ili
kupata uwiano sawa wa habari hii, juzi Jumatatu waandishi wetu
walimtafuta mwanaume aliyetarajiwa kufunga ndoa na Vicky, Charles kwenye
ofisi ya kampuni moja ya simu za mkononi, Kijitonyama jijini Dar lakini
baadhi ya wafanyakazi walisema ana wiki mbili hajakanyaga kazini.
“Huyu bosi hajakanyaga hapa wiki mbili, hayupo,” alijibu mfanyakazi mmoja.
Risasi Mchanganyiko: “Hajakanyaga kivipi? Kasafiri, yuko likizo au?”
Mfanyakazi: “Aliandika barua ya kuomba mapumziko ya wiki mbili kwa hiyo hatujui yuko wapi kwa sasa.”
NYUMBANI KWA VICKY
Baada
ya kutoka ofisini kwa bwana harusi, wanahabari wetu walitinga nyumbani
kwa bibi harusi Vicky Kamata, Sinza ya Vatican, Dar na kukumbana na
mlinzi getini ambaye alisema mgonjwa huyo aliruhusiwa kutoka hospitali
saa mbili usiku wa Jumapili lakini alikuwa amelala na haruhusiwi
kuzungumza na mtu yeyote zaidi ya kupumzika.
“Mheshimiwa karudi jana usiku saa mbili lakini haruhusiwi kuzungumza na watu, amelala,” alisema mlinzi huyo.
CHANZO Global Publishers
Posted by Editor
on 10:18.
Filed under
celebritiesnews,
feature
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0