EAST AFRICAN NEWS

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI LA BOMBA LA MAFUTA GHAFI, WAFUNGUA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA MPAKANI MJINI MUTUKULA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Y...

10 Nov 2017 | 0 comments | Read more

WATANZANIA WANG'ARA SHINDANO LA MWANDISHI BORA WA SAYANSI NA KILIMO AFRIKA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwand...

29 Sep 2017 | 0 comments | Read more
ENTERTAINMENT NEWS

WAZIRI MWAKYEMBE AUDHURIA TAMASHA LA JAMAFEST NCHINI UGANDA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ugand...

14 Sep 2017 | 0 comments| Read more

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI (TASUBA) PAMOJA NA SHORT STATURE OF KENYA ZIKIONYESHA MAIGIZO TAMASHA LA JAMAFEST

 Kikundi cha burudani ya Uchekeshaji kutoka nchini Kenya maarufu kama Short Stature Society of Kenya kikitoa igizo lake la ku...

14 Sep 2017 | 0 comments| Read more

DKT.MWAKYEMBE AMEWAPONGEZA WAJASIRIAMALI WA TANZANIA KWA KUSHIRIKI TAMASHA LA JAMAFEST KAMPALA, UGANDA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia ngoma ya kiutamaduni iliy...

14 Sep 2017 | 0 comments| Read more

WORLD NEWS

TECHNOLOGY

CONGRESS TO SMART DEVICE MAKERS: YOUR SECURITY SUCKS

Four senators propose the "Internet of Things Cybersecurity Improvement Act,"...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

HUAWEI CAME REALLY CLOSE TO SELLING AS MANY PHONES AS APPLE

Apple sold 41 million iPhones in the second quarter, while Huawei's shipments were a...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

SECRET SERVICE WILL REPORTEDLY TEST DRONE FOR TRUMP SECURITY

The Secret Service is looking at whether unmanned aerial vehicles could be use...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

WHAT APPLE'S EARNINGS TELL US ABOUT THE IPHONE 8

The iPhone 7 and 7 Plus may see it's future sibling sooner than many expected.  S...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more
CELEBRITIES NEWS

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan...

09 Sep 2017 | 0 comments| Read more

IMPRESSIVE! BEYONCE LOOKS SLENDER IN LOW-CUT DRESS ON SUSHI DATE IN LA WITH JAY Z

Crazy in love: Beyonce looked absolutely fabulous on a sushi date night with husband Jay Z on Wednesday ...

04 Aug 2017 | 0 comments| Read more

BLOODIED JESSICA BIEL SIZZLES IN STEAMY SEX SCENE WITH HER HUNKY ONSCREEN HUSBAND

Bloody: The gimmick of the show is figuring out why this mother and wife decided to stab a man to death in the first place ...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

Share this Post

SPORTS NEWS

JOSEPH KIMWAGA KUKAA NJE MIEZI MINNE BAADA YA UPASUAJI WA GOTI

WINGA wa Klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga akiwa katika chumba cha matibabu katika Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini ...

06 Sep 2017 | Read more
HEALTH NEWS

PAMOJA NA UNENE LAKINI HAWEZI ACHA KULA

The Brazilian boy, known only as Misael, was born a healthy 6lb 6oz (2.9kg) But every month since, has gained 6lb (3kg), meaning he str...

29 Sep 2014 | Read more
TOP TEN

Top 10 ‘Breaking Bad’ Moments

Ursula Coyote / AMC 10. The ricin’s fate is revealed For all its discussion over the course of the series, ricin had never been ...

08 May 2014 | Read more
FACTS

WACHINA NOMA SANA

 Ukisikia Wachina balaa sasa hii ni moja wapo, Kiwanda Kimojawapo cha China kijulikanacho kwa jina la LandWind kimeibuka na Kutengene...

25 Nov 2014 | Read more
ENVIRONMENT NEWS

A CLIMATE CHANGE INSPIRED PROJECT LAUNCHES IN DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399 ...

04 Aug 2017 | Read more
FASHION

MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA RASMI DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY

. MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige  leo amezindua rasmi  duka ...

12 Jan 2015 | Read more
HISTORY

MAKALA FUPI: Mwanamke aliyehukumiwa kifo Sudan ajifungua

Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuas...

28 May 2014 | Read more
TRAGEDY NEWS

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan...

09 Sep 2017 | Read more

dailyvideo

ISIS yatangaza miliki ya Khalifa Iraq na Syria

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399


Kundi la wapiganaji wa jihadi wanaoongoza mashambulizi nchini Iraq wametangaza miliki ya Khalifa na kuwataka Waislamu wote duniani kutangaza utiifu kwa kiongozi wao.
Kundi hilo la Taifa la Kiislamu la Iraq na Syria ISIS, limejibadili jina na kujiita Tiafa la Kiislamu IS, na kumtangaza Abubakar al-Baghdad kuwa kiongozi wa Waislamu duniani.
Msemaji wa kundi hilo Abu Muhamad Al- Adnan alitagaza kuundwa kwa miliki ya Khalifa na kuchaguliwa kwa Al-Baghdad kuwa Khalifa katika mkanda wa sauti uliyowekwa kwenye mtandao jana Jumapili.
"Baraza la Tiafa la Kiislamu limekutana na kujadili suala hili. Taifa la Kiislamu limeamua kuunda miliki ya Khalifa na kumteua Khalifa wa dola ya Waislamu. Kiongozi wa jihadi Baghdad aliteuliwa kuwa Khalifa wa Waislamu," alisema Al-Adnan.
Msafara wa wapiganaji wa IS mkoan Anbar. Msafara wa wapiganaji wa IS mkoan Anbar.
Kuanzia Iraq hadi Syria
Miliki hiyo ya Khalifa ambayo ni aina ya serikali inayofuata mfumo wa Uislamu ambao ulishuhudiwa mara ya mwisho wakati wa utawala wa Ottoman, inaanzia mkoani Aleppo kaskazini mwa Syria hadi mkoa wa Diyala mashariki mwa Iraq, maeneo ambako kundi hilo limepigana dhidi ya tawala zilizoko madarakani.
Taarifa kutoka mjini Washington zinasema kiongozi wa ISIS Abubakari al-Baghdad alizaliwa mjini Samarra mwaka 1971, na alijiunga na uasi uliyoibuka muda mfupi baada ya uvamizi wa Iraq uliyoongozwa na Marekani mwaka 2003. Vikosi vya Marekani viliamini mwaka 2005 kuwa vilimuuwa Al-Baghdad katika shambulizi la ndege kwenye mpaka wa Iraq na Syria, lakini hilo linaonekana halikuwa sahihi.
Kundi lake limevutia maelfu ya wapiganaji wa kigeni, ambao wanavutiwa na ushawishi wa Baghdad mwenyewe, juhudi la IS kuunda kile inachoamini kuwa ndiyo dola sahihi ya Kiislamu, na mfumo wa kisasa wa propaganda unaotumiwa na kundi hilo, ambao unachapisha majarida na kutoa mikanda ya video kwa Kiingereza na lugha nyingine kadhaa za Ulaya.
Raia wakipeperusha bendera za IS katika mji wa Raqqa nchini Syria. Raia wakipeperusha bendera za IS katika mji wa Raqqa nchini Syria.
Kilifutwa mwaka 1924
Khalifa ndiyo cheyo walichokuwa wanapewa watawala wa Kiislamu tangu alipofariki mtume Muhammad hadi utawala wa Ottoman na kuundwa kwa Jamhuri ya kwanza ya Uturuki mwaka 1924.
Ingawa cheyo hicho kilikuwa kimeundwa kwa ajili ya Khalifa moja na tiafa moja la ukhalifa, nafasi hiyo ilikuwa inazozaniwa mara kwa mara kati ya Waislamu Wasunni na Washia, na wakati mwingine kwa kufuata mipaka ya kijiografia.
IS inapigania kurejeshwa kwa utawala wa zamani wa ukhalifa wa kisunni katika ulimwengu wa kiarabu. Siku ya Jumapili, kundi hilo liliyatolea wito makundi yote kutangaza utiifu kwa khalifa Ibrahmi, ambalo ndiyo jina halisi la Baghdad, hatua ambayo wachambuzi wanaiona kama upinzani wa moja kwa moja dhidi ya Al-Qaeda.
IS iliungana kwa muda mfupi na kundi la Al-Nusra Front, ambalo ni tawi la Al-Qaeda katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini makundi hayo mawili yalivunja uhusiano wote mwezi Februari.
Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki alipokutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry. Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki alipokutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry.
Mashambulizi Tikrit
Jeshi la Iraq lilituma vifaru na magari ya kivita mjini Tikrit siku ya Jumapili, kujaribu kuurejesha mji huo wenye utajiri wa mafuta nguvu ya kijeshi kutoka kwa IS. Msemaji wa jeshi alisema katika madai ambayo hayakuweza kuthibitishwa, kuwa jeshi lilifanikiwa kurejesha uthibiti wa chuo kikuu cha Tikrit na kuwauwa magaidi 70 mjini humo.
Serikali pia ilinunua ndege tano aina ya Sukhoi kutoka nchini Urusi, ambazo ziliwasilishwa mjini Baghdad siku ya Jumamosi, huku televisheni ya serikali ikisema zitatumiwa katika siku zijazo dhidi ya makundi ya kigaidi ya IS.
Jeshi la Iraq limekuwa likitegemea zaidi helikopta za mashambulizi kutokana na kuwa ndege chache sana zinazoweza kutumia makombora ya kisasa. Naibu waziri mkuu anaehusika na masuala ya nishati Hussaini Alshahrishtan, aliilamu Marekani siku ya Jumapili kwa kutofanya vya kutosha kuliimarisha jeshi la Iraq, akisema katika televisheni ya al-Hurra kwamba silaha ziliwasilishwa kwa kuchelewa kuliko ilivyokubaliwa.
Waziri mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu ameiomba jamii ya kimataifa kusaidia mapambano dhidi ya IS Waziri mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu ameiomba jamii ya kimataifa kusaidia mapambano dhidi ya IS
Shinikizo kwa wanasiasa
Wanasiasa mjini Baghdad pia wanashinikizwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yenye uwezo wa kukabiliana na IS; mchakato huu unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne.
"Wakikabiliwa na mgogoro wa kitaifa, viongozi wa kisiasa wa Iraq wanapaswa kuweka maslahi ya taifa na watu wake mbele ya kila kitu," alisema mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladendov katika taarifa siku ya Jumapili, huku kukiwa na ripoti kwamba kundi la waziri mkuu wa zamani Iyad Allawi lenye viti 21 halitahudhuria kikao hicho cha kuundwa serikali.
Huku hayo yakijiri, waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, ameiomba jamii ya kimataifa kuisaidia Jordan kukabiliana na itikadi kali za Kiislamu, na kuunga mkono uhuru kwa Wakurdi wa Iraq.
Matamshi yake yalifuatia ripoti katika vyombo vya habari vya Israel kwamba maafisa mjini Tel Aviv wanahofu kuwa wapiganaji wa Taifa la Kiislamu huenda wakapanua udhibiti wao katika maeneo ya Jordan baada ya Iraq.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe,DW
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman



DW 

Posted by Editor on 14:25. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for ISIS yatangaza miliki ya Khalifa Iraq na Syria

Post a Comment

Photo Gallery

Designed by Solaranlagen | with the help of Bed In A Bag and Lawyers